Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya yapata mkopo wa dola milioni 447.9 kutoka IMF

Baadhi ya watu wanachuna majani chai nchini Kenya huku nchi huo ukihama kuzalisha mazao mengine kwa kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yakitishia mashamba ya chai nchini humo.
CIAT/NeilPalmer
Baadhi ya watu wanachuna majani chai nchini Kenya huku nchi huo ukihama kuzalisha mazao mengine kwa kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yakitishia mashamba ya chai nchini humo.

Kenya yapata mkopo wa dola milioni 447.9 kutoka IMF

Ukuaji wa Kiuchumi

Bodi tendaji ya Shirika la fedha duniani IMF imekamilisha awamu ya nne ya Ukaguzi wa Mpango wa Upanuzi wa Hazina kwa taifa la Kenya na kuipa nchi hiyo mkopo wa dola milioni 447.9 ili iweze kutekeleza mipango yake ya upanuzi na usaidizi wa mikopo.

“Kenya imepata takriban dola milioni 450 leo kutoka kwa IMF ni Mary Goodman, Mwakilishi wa IMF nchini kenya akitoa taarifa rasmi ya taifa hilo kupokea mkopo unaolenga kusaidia nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuhimili majanga yanayosumbua dunia kwa sasa ikiwemo ukame, changamoto zilizosababishwa na COVID-19, Kuimarisha utawala bora na mageuzi mapana ya kiuchumi.

Anasema mkopo huu umefanya ukubwa wa mpango wa IMF nchini Kenya kufikia takriban dola bilioni 2.4 na haya yote yanawezekana kwakuwa fedha zinazotolewa kwa nchi hiyo zimeonekana kuleta matokeo.

Bi. Goodma amesema “Kuongezeko la ukusanyaji kodi na uangalifu kwenye matumizi, hatua hizi zina imarisha deni kama sehemu ya Pato la Taifa GDP lipo chini ya viwango vilivyotarajiwa. Kenya ilifanikisha hili kwa sababu utawala wa Rais wa Kenya William Ruto imejitolea kwa nguvu kukabili bili zilizosalia za mwaka jana na matumizi yasiyokuwa na bajeti kuanzia mapema mwaka huu. Walichukua hatua ya ujasiri. Walimaliza kabisa ruzuku ya mafuta ya petroli, na wanatafuta kila sehemu namna ya kuokoa gharama ili kushikilia nakisi ya mwaka huu iwe chini ya kiwango kilichowekwa kwenye bajeti.”

Uwazi kwenye kandarasi zinazotolewa na serikali pia ni eneo jingine Mwakilishi huyu wa IMF alilogusia na kusema “Katika mapitio yaliyo fanywa na IMF yameona maendeleo katika utawala. Kuna maelezo mapya kuhusu wamiliki wa makampuni yanayoshinda kandarasi za serikali na yanachapishwa kwenye tovuti ya ununuzi wa umma. Hata hivyo kazi zaidi bado iko ya kuimarisha mfumo wa Kenya wa kupambana na ufujaji wa fedha na kurekebisha makampuni ya serikali.

Pamoja na kumwagiwa sifa kwenye kufanikiwa katika ajenda ya mageuzi ya kimuundo, bado kuna ucheleweshaji fulani.

“Changamoto bado zipo, ingawa Kenya bado inakabiliwa na bei ya juu ya kimataifa ya chakula na mbolea, na dola ya Marekani nayo imekuwa na nguvu sana dhidi ya sarafu nyingi za kimataifa. Katika kipindi hiki kigumu, sera ya fedha na kubadilika kwa viwango vya ubadilishaji fedha vina jukumu kubwa la kutekeleza. Hatua za kufufua soko la fedha za kigeni pia ni muhimu na zitasaidia kusaidia hifadhi ya fedha za kigeni nchini Kenya. “