Katika kampeni ya aina yake dinosaur awasihi viongozi wa dunia kutochagua kutoweka

Katika filamu fupi ya UNDP, dinosaur aitwaye Frank amewasihi viongozi wa dunia kutochagua kutoweka kwa viumbe
UNDP
Katika filamu fupi ya UNDP, dinosaur aitwaye Frank amewasihi viongozi wa dunia kutochagua kutoweka kwa viumbe

Katika kampeni ya aina yake dinosaur awasihi viongozi wa dunia kutochagua kutoweka

Tabianchi na mazingira

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP leo limezindua kampeni mpya na ya aina yake kwa ajili ya kuchagiza hatua dhidi ya janga la mabadiliko ya tabianchi. 

Kampeni hiyo iliyozinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kwa mara ya kwanza, dinosaur mkali na anayezungumza ameingia ndani ya Ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na kutoa onyo kali kwa wanadiplomasia wowote ambao bado wanafikiri hatua dhjidi ya mabadiliko ya tabianchi ni kwa ajili ya Ndege tu. 

"Angalau tulikuwa na asteroid," dinosaur hiyo mla nyama anaonya, akimaanisha nadharia maarufu inayoelezea kutoweka kwa dinosaur miaka milioni 70 iliyopita. Akiwaulina “Kisingizio chako ni nini?” 

Dinosaur huyo si wa maisha halisi bila shaka, bali ni esehemu muhimu iliyotengenewa kwa kompyuta kutoka kwenye filamu fupi mpya iliyozinduliwa jana na na UNDP kama kitovu cha kampeni yao ya 'Usichague Kutoweka'.  

Dinosaur huyo kisha akaiambia hadhira ya wanadiplomasia waliotaharuki kwamba "Ni wakati wa wanadamu kuacha kutoa visingizio na kuanza kufanya mabadiliko" kushughulikia janga la mabadiliko ya tabianchi.” 

Katika filamu fupi ya UNDP, dinosaur aitwaye Frank amewasihi viongozi wa dunia kutochagua kutoweka kwa viumbe
UNDP
Katika filamu fupi ya UNDP, dinosaur aitwaye Frank amewasihi viongozi wa dunia kutochagua kutoweka kwa viumbe

Utengenezaji wa filamu hiyo 

 Ni filamu ya kwanza kabisa kutengenezwa ndani ya Ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  kwa kutumia taswira inazotengenezwa na kompyuta, inayojulikana kama CGI, na imetumia watu mashuhuri duniani kuweka sauti ya dinosaur huyo katika lugha nyingi, wakiwemo waigizaji Eiza González (Kihispania), Nikolaj Coster-Waldau (Kidenishi) , na Aïssa Maïga (Kifaransa). 

Leo pia UNDP imetoa utafiti wake kama sehemu ya kampeni unaonyesha kuwa dunia inatumia dola bilioni 423 kila mwaka kutoa ruzuku ya nishati ya mafuta kisukuku, kiasi cha kutosha kugharamia chanjo ya COVID-19 kwa kila mtu duniani au mara tatu ya kiwango kinachohitajika kwa mwaka ili kutokomeza umaskini uliokithiri duniani. 

"Fikiria mambo mengine yote unayoweza kufanya kwa pesa hizo. Ulimwenguni kote watu wanaishi katika umaskini. Je, hufikirii kuwa kuwasaidia kungekuwa na maana zaidi kuliko kulipia kuangamia kwa viumbe vyenu vyote?” Amesema dinosaur huyo.