Mabadiliko ya tabianchi yanaweza kuwa mbaya kama saratani katika baadhi ya nchi duniani: UNDP
Bila hatua za pamoja na za haraka, mabadiliko ya tabianchi yatazidisha ukosefu wa usawa na kupanua pengo katika maendeleo ya binadamu kulingana na jukwaa jipya lililopewa jina “Human Climate Horizons” lililozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na maabara ya athari za mabadiliko ya tabianchi.