Japan 'yapiga jeki' elimu ya sayansi miongoni mwa wakimbizi, Uganda

7 Novemba 2019

Katika kuitikia wito wa Umoja wa  Mataifa wa kusaidia wakimbizi na jamii zinazowahifadih kupata elimu, nchini Uganda, serikali ya Japani imekamilisha ujenzi wa maabara ya sayansi kwenye shule ya secondari ya Kyangwali katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali na kuikabidhi kwa jamii husika. John Kibego na maelezo Zaidi.

Shamra shamra kwenye uzinduzi wa jengo hili la maabara lenye vyumba vitatu – cha somo la Kemia, Fizikia na  Bayolojia. Ujenzi wake umegharimu serikali ya Japani shilingi milioni 270 za Uganda sawa na dola 80,000 za Kimarekani.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kyangwali, Patrick Isingoma amepata matumaini ya wanafunzi wake kufuzu katika masomo ya sayansi akisema, “katika Nyanja ya sayansi tulikuwa tunakosa mengi hasa maabara. Lakini baada ya uzinduzi wa maabara hii natumai kuwa mtindo wa elimu hiyo utainuka”

Naye Ruslan Shabdunov Afisda wa Ulinzi wa wakimbizi katika shirika la Umoja wa Matifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) kwenye makaazi ya wakimbizi ya Kyangwali, ameipongeza Japani akisema mchango huu ni muhimu kwa wanafunzi wakimbizi pamoja na wenyeji Zaidi ya 600 wa shule hiyo pekee ya sekondari iliyomo kambini. Ameongeza kuwa, “tangu 1997 hadi leo, hapakuwa na baabara ya sayansi na hivyo tunafurahi sana leo kushuhudia uzinduzi wa maabara hii na Balozi wa Japana. Tunatumai kuwa itasaidia wakimbizi na jamii za wenyeji kufikai haki yao ya elimu bora”

Kazuaki Kameda ni Balozi wa Japani nchini Uganda ambaye amesema kuwa, “hii ni miongoni mwa shule zilizofurika Zaidi nilizowahi kushuhudia na sishangai. Japan kama mwanachama wa jamii ya kimataifa anayewajibika, tunachukua hatua kutoa msaada na tumekuwa tukiunga mkono jamii hizi na wenyeji”

Na mwanafunzu mnufaika hakuficha hisia zake.

Mwaka 2017 Uganda ilipitisha masomo ya sayansi matatu ya matatu biolojia, kemia na Fisikia kuwa masomo ya lazima kama njia ya kuinua elimu ya sayansi kote nchini.

Lakini miundombinu na vifaa sitahili kuwezesha ndoto hiyo, vimesalia katika uhaba kwenye shule za serikali na zile za kipekee.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter