Jopo laundwa ili kutokomeza magonjwa yasiyoambukizwa: WHO

Mgonjwa anaandaliwa kwa ajili ya matibabu ya saratani katika hospitali huko Kandy, Sri Lanka
Shirika la afya duniani-WHO limetangaza kuundwa kwa jopo jipya la ngazi za juu ili kuweza kuchagiza hatua za kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukizwa NCDs, ambayo yameelezwa kuwa moja ya yaliyo mstari wa mbele kwa vifo vya binadamu. Magonjwa hayo ni kama vile saratani, ugonjwa wa moyo, mapafu na kisukari.