Mameya kutoka miji 50 duniani wakutana London kujadili NCDs na majeraha: WHO

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO limesema mameya na maafisa wengine kutoka zaidi ya miji 50 kote duniani wanakutana London Uingereza kuanzia leo Machi 14 hadi Machi 16 kushughilikia magonjwa yasio ya kuambukiza NCDs na kuzuia majeraha, katika mkutano wa kwanza wa ushirikiano kwa ajili ya miji yenye afya.
Tangu ushirikiano huo kuanzishwa mwaka 2017wajumbe wa mtandao wa kimataifa wa miji 70 wamekuwa wakitekeleza miradi na kuchagiza sera imara za afya ya umma katika Nyanja mbalimbali ikowemo kudhibiti tumbaku, sera za chakula, usalama barabarani, kuimarisha ufuatiliaji wa NCDs na kuzuia watu kutumia kiwango cha kupitiliza cha dawa.
WHO inasema magonjwa yasiyoambukiza ikiwa ni pamoja na magonjwa ya moyo, saratani, kisukari na magonjwa sugu ya kupumua na majeraha yanasababisha asilimia 80 ya vifo vyote ulimwenguni.
Huku idadi kubwa ya watu duniani sasa wakiishi katika mazingira ya mijini, miji shirika hilo linaongeza kuwa viongozi wa miji hiyo wako katika nafasi ya kipekee ya kubadilisha mapambano dhidi ya NCDs na majeruhi na kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika kwa kutekeleza sera ambazo zimethibitishwa kuzuia kukabiliwa na hatari.
Tangu ushirikiano wa miji yenye afya ulipoanzishwa mwaka wa 2017, wanachama wa mtandao wa kimataifa wa miji 70 wamekuwa wakitekeleza miradi inayoungwa mkono na ushirikiano huo na kupigia chepuo sera kali za afya ya umma katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na udhibiti wa tumbaku, sera ya chakula, usalama barabarani, kuimarisha ufuatiliaji wa NCDs na kuzuia watu kutumia dawa kiasi cha kupindukia.