Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatuwezi kusubiri hadi baa la njaa litangazwe tunafanya kila tuwezalo kuwanusuru Wasomali:WFP 

Mama na mwanae katika kituo cha afya cha kutibu utapiamlo nchini Somalia
© UNICEF/Sebastian Rich
Mama na mwanae katika kituo cha afya cha kutibu utapiamlo nchini Somalia

Hatuwezi kusubiri hadi baa la njaa litangazwe tunafanya kila tuwezalo kuwanusuru Wasomali:WFP 

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limekuwa mstari wa mbele nchini Somalia likifanya kila liwezekanalo kufikisha msaada wa kuokoa maisha kwa takriban watu milioni 3.7 walio katika hatihati ya baa la njaa, huku zaidi ya 300,000 miongoni mwao wakipatiwa msaada wa lishe. Hata hivyo shirika hilo limeonya kwamba hatua Madhubuti zisipochukuliwa sasa baa la njaa haliepukiki. Leah Mushi na taarifa zaidi 

Picha zilizopigwa toka angani katika maeneo ya vijijini ya Galkayo jimboni Galmadug zinadhihirisha hali mbaya ya ukame na mifupa ya mifugo iliyokufa kwa kukosa maji na njaa imepatakaa. 
Ukame huu uambao haujawahi kuhushudiwa umeikumba nchi nzima ya Somalia na kusambabisha madhara makubwa, ikiwemo utapiamlo wa hali ya juu au unyafuzi kwa watoto ambao wengi inabidi wapatiwe tiba kwenye vituo maalum bvya lishe. 
WFP imeonya kuwa kuna kila dalili baa la njaa kutoepukika Somalia endapo hatua za haraka hazitochukuliwa sasa. Naibu mkurugenzi wa WFP Somalia Bainmankay Sankoh anazsisitiza hilo "Njaa nchini Somalia imekaribia sana kuliko hapo awali, ni ukweli ulio bayana endapo hatutachukua hatua mara moja. Kama WFP tunajua kutokana na uzoefu kwamba hatuwezi kusubiri tamko rasmi la baa la njaa kuchukua hatua. Kwa hivyo kwa miezi kadhaa tumekuwa tukifanya kazi ili kuongeza msaada wetu wa kuokoa maisha nchini Somalia. Tunawafikia watu wengi zaidi kuliko tulivyowahi kuwafikia hapo awali. Watu milioni 3.7 tumewafikia na msaada ni zaidi ya mara mbili ya idadi tuliyofikia mwezi wa Aprili  na wengine zaidi ya 300,000 kwa msaada wa lishe.” 
Katika eneo la Hudur WFP imeweka kituo maalum cha lishe ambapo watoto wanapimwa utapiamlo na kupewa chakula cha matibabu kilichotengenezwa kwa karanga. 
Na kwa mamilioni ya wakimbizi wa ndani kama Canab Mohamed mama wa Watoto 9 alityekimbia machafuko pamoja na mumewe mjini Bacakweyne na kuishia kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani karibu na Galkayo WFP inawapatia chakula na fedha taslim zinazowaruhusu kununua vyakula kama mbogamboga, matunda na nyama. 
Kwa mujibu wa WFP baa la njaa linatarajiwa kati ya mwezi Oktoba na Desemba katika wilaya za Baidoa, Burkhaba na kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani kwenye jimbo la Bay kama msaada hautoongezwa haraka. 
Mra ya mwisho baa la njaa liliikumba Somalia mwaka 2011-2012 na lilikatili maisha ya zaidi ya watu 250,000.