Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali si hali tena Somalia:Mashirika ya kibinadamu ya UN

Ibrahim mtoto wa miezi 8 anayeugua utapiamlo akifanyiwa vipimo katika hospitali ya Moghadishu Somalia
© UNICEF/Omid Fazel
Ibrahim mtoto wa miezi 8 anayeugua utapiamlo akifanyiwa vipimo katika hospitali ya Moghadishu Somalia

Hali si hali tena Somalia:Mashirika ya kibinadamu ya UN

Msaada wa Kibinadamu

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yamesema Somalia imefikia kkatika hali mbayá sana. Maisha ya mamia ya maelfu ya watu yamo hatarini hivi sasa kutokana na tathimini iliyofanywa hivi karibuni kuhusu uhakika wa chakula na lishe.

Baa la njaa linajitokeza katika wilaya za Baidoa na Burkhakaba kwenye jimbo la Bay lina uwezekano wa kudumu hadi Machi 2023 ikiwa msaada wa kibinadamu hautaongezwa kwa kiasi kikubwa na mara moja.

Mashirika hayo yameongeza kuwa mamilioni zaidi wanakabiliwa na viwango vikali vya njaa kali huku wanawake, hasa wajawazito na wanaonyonyesha, na watoto wa chini ya umri wa miaka mitano ni miongoni mwa walio katika hatari zaidi na wanahitaji usaidizi wa haraka ili kuepusha zahma kubwa.

Njaa na vifo kuna uwezekano mkubwa tayari vinatokea yamesema mashirika hayo yakikumbusha kuwa wakati wa njaa ya mwaka 2011, karibu zaidi ya asilimia 50 ya watu 250,000 waliokufa, walikufa kabla ya tamko rasmi la baa la njaa na takriban nusu walikuwa watoto.....