Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumieni chanjo zilizopo kukabiliana na viua vijiumbe maradhi: WHO

Usugu wa dawa za viuavijumbemaradhi (AMR) unatishia uzuiaji thabiti na matibabu ya maambukizi yanayosababishwa na vijidudu mbalimbalimbali.
Picha: WHO
Usugu wa dawa za viuavijumbemaradhi (AMR) unatishia uzuiaji thabiti na matibabu ya maambukizi yanayosababishwa na vijidudu mbalimbalimbali.

Tumieni chanjo zilizopo kukabiliana na viua vijiumbe maradhi: WHO

Afya

•    WHO yataka chanjo zilizopo sasa zitolewa kimataifa kwa usawa
•    WHO yataka uharakishwaji wa mchakato wa upatikanaji wa chanjo
•    Utengenezaji wa chanjo uharakishwe kama ilivyokuwa kwenye chanjo za COVID19

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limetoa wito wa matumizi ya chanjo zilizopo pamoja na hitaji la kuharakisha majaribio ya chanjo mpya zinazotengenezwa kwa sasa kwa ajili ya kukabiliana na dawa sugu dhidi ya viua vijiumbe maradhi, AMR. 
 
Wito huo umetolewa leo jijini Geneva Uswisi wakati kwenye ripoti ya kwanza ya aina yake ya shirika hilo juu ya uchambuzi wa chanjo zinazotengenezwa ambapo imebainishwa mpaka sasa zaidi ya chanjo 60 ziko katika hatua mbalimbali za vipimo vya kliniki ikiwa ni pamoja na kadhaa kuwa katika hatua za mwisho ili kuweza kutolewa kwa majaribio kwa magonjwa yaliyopewa kipaumbele katika orodha iliyotolewa na WHO. 

Dkt. Hanah Balkhy, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa AMR amesema “Kuzuia maambukizi kwa kutumia chanjo kunapunguza matumizi ya viuavijasumu, ambayo ni moja ya vichocheo vikuu vya vimelea sugu vya ya vijiumbe maradhi. Hata hivyo bado kati ya vimelea sita vya juu vya ya vijiumbe maradhi vinavyosababisha vifo kutokana na AMR ni ugonjwa mmoja tu wenye chanjo ambao ni Pnuemoccocal” 

Amebainisha kuwa upatikanaji wa bei nafuu na kwa usawa wa chanjo za kuokoa Maisha kama vile dhidi ya ugonjwa wa pneumococcus unahitajika haraka kuokoa maisha na kupunguza ongezeko la AMR. 

Sampuli kutoka kwa kuku ikichambuliwa nchini Kenya kama sehemu ya utafiti kuhusu bakteria sugu ya dawa.
© FAO/Luis Tato
Sampuli kutoka kwa kuku ikichambuliwa nchini Kenya kama sehemu ya utafiti kuhusu bakteria sugu ya dawa.

Janga la Kimya kimya

Mgonjwa anapobainika kuwa na AMR ni kwamba ana zaidi ya maambukizi ya bakteria. AMR hutokea wakati ambapo bakteria, virusi, fangasi na vimelea vingine hubadilika baada ya muda na dawa kushindwa kutibu. Wakati mtu anapata maambukizi ya vijidudu hivi ambayo yanaelezwa kuwa sugu kwa dawa mara nyingi huelezwa kuwa ni ngumu kutibu. 

Shirika hilo limeeleza ya vijiumbe maradhi ni janga la kimya kimya linaloleta wasiwasi mkubwa kwa afya ya umma ambapo takwimu za mpaka sasa zinaonesha maambukizi sugu ya vijiumbe maradhi pekee anahusishwa na takriban vifo million 4.95 kwa mwaka na vifo milioni 1.27 vinahusishwa moja kwa moja na AMR. 

Dkt. Hanan Balky, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha AMR katika Shirika la Umoja wa Mataifa la  Afya Duniani.
WHO
Dkt. Hanan Balky, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha AMR katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani.

Ziharakishwe kama chanjo za COVID19

Pamoja na ukweli kwamba chanjo za AMR haziwezi kupatikana katika kipindi kifupi kutokana na mchakato wa utengenezaji wake kuchukua zaidi ya miaka 10 mpaka 15 lakini WHO imetaka hatua mbadala kuchukuliwa haraka ili kuzuia maambukuzu sugu kutokea pamoja na kuhimiza upatikanaji sawa na wa kimataifa kwa chanjo ambazo tayari zipo hasa miongoni mwa watu wenye uhitaji zaidi na walio katika mazingira yenye rasilimali chache. 

“Njia mbadala zinapaswa kupatikana ili kuharakisha mchakato wa kuharakisha maendeleo ya utengenezajiwa chanjo. Funzo tulilo pata kutokana na utengenezaji wa chanjo za COVID-19 na chanjo ya mRNA linatupa fursa ya kipekee la kutafuta kutengeneza chanjo dhidi ya ya vijiumbe maradhi.” Amesema Dkt. Haileyesys Getahun ambaye ni Mkurugenzi wa WHO Idara ya uratibu wa AMR duniani. 

Kauli yake imeungwa mkono na Mkuu wa Idara ya Kinga, chanjo na kibiolojia wa WHO Dkt. Kate O’Brien ambaye ameeleza “Lazima tutumie mafunzo tuliyopata wakati wa janga la COVID-19 na kuharakisha utafutaji wa chanjo za kushughulikia AMR. Utengenezaji wa chanjo ni ghali, na kuna changamoto za kisayansi ambazo mara nyingi zinakuwa na viwangov ya juu vya kushindwa na wale wanaofaulu kunakuwa na mahitaji tata ya udhibiti na utengenezaji yanayohitaji muda zaidi.”

Ripoti hiyo inachunguza baadhi ya changamoto zinazokabili uvumbuzi na maendeleo ya chanjo. 
Kusoma kwa undani kuhusu ripoti hiyo bofya hapa