Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Wakazi waliosalia Mariupol walikwa wakitumia choo kimoja wakati mji ulikuwa ukiendelea kushambuliwa.

Ukraine: Operesheni ya Umoja wa Mataifa na Msalaba Mwekundu inaendelea kuwahamisha raia kutoka kwenye kiwanda kilichoathiriwa cha Mariupol

© Alina Beskrovna
Wakazi waliosalia Mariupol walikwa wakitumia choo kimoja wakati mji ulikuwa ukiendelea kushambuliwa.

Ukraine: Operesheni ya Umoja wa Mataifa na Msalaba Mwekundu inaendelea kuwahamisha raia kutoka kwenye kiwanda kilichoathiriwa cha Mariupol

Msaada wa Kibinadamu

Operesheni ya Umoja wa Mataifa na Shirika la Msalaba Mwekundu (ICRC) ya kuwaondoa raia waliokata tamaa baada ya kukwama katika kiwanda cha chuma cha Azovstal katika mji wa bandari wa Mariupol nchini Ukraine inaendelea, amethibitisha Msemaji wa ofisi ya masuala ya kibinadamu nchini humo Jumapili.

"Operesheni ya kupita kwa usalama…inaendelea leo", alisema Saviano Abreu, wa OCHA nchini Ukraine, na kuongeza kuwa juhudi “zinaratibiwa” na Umoja wa Mataifa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, “kwa uratibu na pande zinazohusika katika mzozo. .”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika vyombo vya habari, zaidi ya raia 100 waliruhusiwa kuondoka katika awamu ya kwanza ya operesheni hiyo.

Bw. Abreu alisema mamlaka ya Urusi na Ukraine zimekubali kwamba raia ambao wamekuwa katika kiwanda cha chuma kilichoharibiwa kwa karibu miezi miwili, "wanawake, watoto na wazee", watahamishwa hadi Zaporizka, ambako kuko chini ya udhibiti wa Ukraine. kaskazini mwa Mariupol.

Arthur mwenye umri wa miaka mitano kutoka Mariupol, Ukraine, angali ana makovu baada ya kunusurika njaa na kulipuliwa kwa mji alikozaliwa
© UNICEF
Arthur mwenye umri wa miaka mitano kutoka Mariupol, Ukraine, angali ana makovu baada ya kunusurika njaa na kulipuliwa kwa mji alikozaliwa

Msaada kwa waathirika

Huko, "watapata msaada wa haraka wa kibinadamu, ikiwa ni pamoja na huduma za kisaikolojia", alisema Abreu. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) nchini Ukraine, liliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba wao na mashirika mengine washirika, walikuwa "tayari kupokea watu waliohamishwa", na wakitumai kwamba "uhamisho zaidi utafuata".

Katibu Mkuu António Guterres alisafiri hadi Moscow na kukutana na Rais Vladimir Putin mapema wiki iliyopita, na kufanya makubaliano kutoka kwa Waziri Mkuu wa Urusi "kimsingi" kuruhusu operesheni ya kuokoa maisha ya wikendi hii, baada ya wiki za majaribio kushindwa kutoa njia salama ya uhamishaji wa watu wengi.

Baada ya kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika mji mkuu wa Kyiv siku ya Alhamisi, umuhimu wa haraka wa kukomesha kile Bwana Guterres aliita "mgogoro ndani ya mgogoro" wa hatimaye kuruhusu raia kuondoka katika mji ulioharibiwa wa pwani baada ya wiki za mashambulizi ya Urusi, ilikuwa mada ya "majadiliano makali" kati ya pande hizo mbili.

Uharibifu uliosababishwa na makombora huko Mariupol, kusini mashariki mwa Ukraine.
© UNICEF/Evegeniy Maloletka
Uharibifu uliosababishwa na makombora huko Mariupol, kusini mashariki mwa Ukraine.

Usalama wa raia, jambo kuu

Bwana Abreu alisema katika taarifa kwa waandishi wa habari iliyotolewa Jumapili kwamba, operesheni hiyo imeanza kwa msafara wa Umoja wa Mataifa na Msalaba Mwekundu kuondoka kuelekea Mariupol siku ya Ijumaa, kutoka Zaporizka, safari ya takriban kilomita 230.

"Kwa kuwa operesheni bado zinaendelea, hatutatoa maelezo zaidi kwa wakati huu," alisema, "kuhakikisha usalama wa raia na wasaidizi wa kibinadamu kwenye msafara huo."

Alihitimisha akisema kwamba Umoja wa Mataifa "utaendelea kushinikiza njia salama nje ya jiji la Mariupol kwa raia wote wanaotaka kuondoka. Umoja wa Mataifa unashirikiana kikamilifu na wahusika kuendeleza juhudi hizi."

Iwapo waliohamishwa wanaweza kufikia usalama, itakuwa ni mara ya kwanza kwa msafara ulioandaliwa na mashirika ya kibinadamu kuweza kuwalinda raia, ambao wamekuwa wakiishi kwa kupigwa risasi na silaha kali za Urusi na mashambulizi ya angani, tangu siku za kwanza za uvamizi wa Urusi.

Idadi ya vifo ndani ya Mariupol haijulikani, lakini meya wa jiji hilo ameripoti kuwa zaidi ya raia 20,000 wameuawa.

Wanajeshi wa mwisho wa Ukraine waliosalia wakilinda jiji, wamejificha ndani ya majengo makubwa ya chuma ya enzi ya Usovieti - pamoja na mamia ya raia.