Miezi miwili baada ya machafuko, hofu yaendelea kutawala Ituri DRC

Machafuko katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC yansababisha watu kukimbilia nchi jirani.
UNICEF/Madjiangar
Machafuko katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC yansababisha watu kukimbilia nchi jirani.

Miezi miwili baada ya machafuko, hofu yaendelea kutawala Ituri DRC

Amani na Usalama

Ikiwa ni miezi miwili tangu kuzuka kwa machafuko yaliyowalazimisha maelfu ya watu kufungasha virago na kuzikimbia nyumba zao huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwenye jimboi la Ituri hofu bado imetanda katika jimbo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo, upungufu mkubwa wa ufadhili na ongezeko la kutokuwepo na usalama, kuna maanisha ni kuongezeka haja ya msaada wa mahitaji ya kibinadamu hali ambayo imewafanya watu washindwe kurejea nyumbani.

Akizungumza na waandhishi wa habari mjini Geneva, Uswisi msemaji wa UNHCR Babar Baloch amesema katika wiki tatu za mwisho za mwezi wa Juni pekee zaidi ya watu wapya 145,000 wametawanywa na kwenda kusaka usalama na msaada katika makazi ya wakimbizi wa ndani yaliyoko Ituri, huku wengine 215,000 zaidi wakikadiriwa kukimbilia maeneo ya jirani.”

Ameongeza kuwa hata hivyo hiyo huenda isiwe idadi kamili kutokana na ugumu wa kufika baadhi ya maeneo ambako watu wamekimbilia na maelfu wameendelea kukimbia tangu wakati huo ingawa ni kwa kiwango kidogo.

Baloch amesisitiza kuwa “kuendelea kwa machafuko baina ya makundi ya wanamgambo kuna maanisha watu wengi wanaogopa kurejea nyumbani. Katika ziara ya karibuni kwenye mji wa Djugu kutoa msaada wafanyakazi wa UNHCR walikuwa vijiji vikiwa bila watu, idadi kubwa ya nyumba zilizochomwa na nyumba zilizotelekezwa”

UNHCR inasema kutokana na hali hiyo watu wamelazimika kutafuta malazi kokote wawezako baadhi wamehifadhiwa na ndugu wa familia lakini wengi wamelazimika kulala nje katika maeneo ya wazi ikiwemo katika mji mdogo wa Drodro ambao katika wiki chache umeshuhudia idadi ya watu ikiongezreka mara tatu huku shule na makanisa vikigeuzwa kuwa mabweni ya kulala.

Wakimbizi wamekuwa wakisimulia madhila makubwa ikiwemo mauaji ya ndugu zao ambao walijaribu kurejea kwenyda kuchukua vitu vyao na chakula huku onyo likitolewa na wanamgambo la watu kutorejea. Hofu ya mustakabali wa wato hao imetawala na mahitaji ya haraka zaidi kwa mujibu wa UNHCR ni malazi, maji, usafi, huduma za afya na chakula.

Na mrundikano katika makazi hayo ya muda umeelezwa kuwaweka wanawake na wasichana katika hatari kubwa ya ukatili wa kijinsia na wa kingono, huku ukosefu wa maji safi wanawaweka watu hao katika hatari ya mlipuko na kusambaa kwa magonjwa.

UNHCR inasisitiza kuwa ufadhili wa mahitaji hayo ya kibinadamu ni muhimu sana kwani hadi sasa UNHCR imepokea asilimia 32 tu ya dola milioni 150 inazohitaji kwa ajili ya operesheni za kibinadamu nchini DRC.