Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taka zitokanazo na COVID-19 zaiongezea mzigo Afrika- WHO 

Taka za matibabu.
UNEP
Taka za matibabu.

Taka zitokanazo na COVID-19 zaiongezea mzigo Afrika- WHO 

Afya

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limeonya kwamba vifaa vya kukabiliana na janga la COVID-19 kama barakoa, glovu, vifaa vingine vya kinga ya binafsi na Chanjo vimeenea kila mahali barani Afrika wakati wa janga la COVID-19 kama kinga dhidi ya virusi yenyewe, lakini pia kama taka za matibabu, zikilemea dampo za Afrika ambazo tayari zimefurika. 

Kwa mujibu wa WHO kabla ya kuanza kwa janga hili, Afrika ilizalisha takriban tani 282,000 za taka za matibabu kila mwaka, kulingana na ripoti ya 2021 iliyochapishwa na jariuda la sage kuhusu usimamizi wa taka zinazosababisha wa matibabu . 

Sasa, nchi nyingi zinaripoti ongezeko la taka za matibabu hadi mara tano zaidi. 

Ili kukabiliana na ongezeko hilo, WHO inazisaidia nchi za Kiafrika kuweka itifaki maalum za udhibiti wa taka na zinazoendana na hatua zilizopo.  

Hizi ni pamoja na kukuza mbinu salama za utupaji taka ambazo zinawezekana, zinazozingatia  masuala ya kiuchumi na endelevu. 

"WHO inashiriki katika juhudi za sekta mbalimbali kuleta mabadiliko katika mifumo ya udhibiti wa taka barani Afrika," anasema Claude Mangobo, afisa wa masuala ya kiufundi ya Chanjo na mnyororo wa ugavi katika kityengo cha chanjo cha ofisi ya kanda ya Afrika ya WHO . 

Ameongeza kuwa "Ni mchakato muhimu ambao tumejitolea kwa afya ya bara hilo na watu wake." 

Chanjo zilizokwishatolewa Afrika 

WHO inasema huku kukiwa na zaidi ya chanjo milioni 435 za COVID-19 zilizokwisha tolewa na kusambazwa  barani Afrika hadi sasa ukiwa ni utolewaji mkubwa zaidi wa chanjo ya aina yoyote katika historia ya bara hilo, haja ya utupaji bora wa taka za matibabu imekuwa muhimu zaidi na dharura kwa sasa. 

Katika kanda ya Afrika, barakoa, glovu na vifaa vya kinga vimekuwa sare ya kila siku, haswa miongoni mwa wafanyakazi wa afya.  

Ni kati ya asilimia 75% ya taka za matibabu zinazohusiana na COVID-19 ambazo sio hatari zinaposhughulikiwa ipasavyo. 

Lakini, asilimia 25% iliyobaki ya vifaa hivyo ni taka hatari za chanjo ya COVID-19. Hizo zinajumuisha chupa za chanjo ya COVID-19 zilizotupwa na makasha ya kuhifadhi mbomba ya sindano hizo na taka nyingine zenye makali. 

Uhifadjhi uliosanifiwa vyema na madampo masafi yalizotengenezwa kwa uhandisi wa hali ya juu yanapendekezwa.  

Hata hivyo, WHO inasema katika nchi nyingi kuna mapungufu makubwa katika matumizi ya miongozo ya usimamizi wa taka.  

Ikiwa hazipo, hatua kama vile kuchoma taka kwenye shimo lililojitenga au kuzichimbia kwa usalama kwenye majengo ya hospitali ni vyema zaidi kuliko kutupa hovyo au ni mbaya zaidi, kuchoma taka kwenye mapipa au mahali pa wazi, na kusababisha uzalishaji wa moshi wenye sumu. 

Matumizi ya teknolojia 

Kwa mujibu wa mikataba ya Basel ya 1989 na Stockholm wa 2001 inayosimamia udhibiti wa taka za matibabu, WHO inatetea matumizi ya teknolojia ambazo hazizalishi na kutoa kemikali au moshi wa hatari, kama vile uchomaji kwa kutumia joto la juu, kwa kutumia mvuke wa kiwango cha au microwave. 

Hata hivyo, tathmini ya hivi kribuni ya WHO katika nchi 10 za Afrika imebaini kuwa ni nchi nne pekee zilizopata zaidi ya asilimia 80% katika usimamizi wao wa taka za COVID-19, ambao ni pamoja na utunzaji wa sindano zilizotumika, kuhifadhi na kutoa na kuhifadhi makasha yanayohifadhi sindano hizo, kurekodi majeraha yatokanayo na sindano, kuhifadhi na kuondoa vifaa vilivyotumika  kuhifadhi chanjo, kusimamia eneo la kuhifadhia taka, na kutupa taka za chanjo kwenye maeneo husika. 

Ripoti ya WHO mwezi Februari iligundua kuwa asilimia 60% ya vituo vya huduma za afya katika nchi zinazoendelea havina vifaa vya kushughulikia taka zilizopo, achilia mbali mzigo wa ziada wa COVID-19.  

WHO inasema “Hii inaweza kuwaweka wahudumu wa afya kwenye hatari ya majeraha ya sindano, kuungua na kuambukizwa viini vya magonjwa. Pia ina athari mbaya kwa jamii zinazoishi karibu na madampo yasiyosimamiwa vizuri na maeneo ya kutupa taka kupitia hewa iliyochafuliwa kutokana na taka zinazoungua, ubora duni wa maji au wadudu wanaobeba magonjwa.” 

Hatua zinazochukuliwa 

Ili kukabiliana na hali hiyo, WHO, pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP,  Global Environment Facility, Makundi ya uhifadhi wa mazingira, na shirika lijulikanalo kama Health Care Without Harm, shirika linalofanya kazi kwa ajili ya utunzaji wa afya unaozingatia mazingira wamebuni mfumo wa maamuzi wa kuwasaidia wafanyakazi wa afya kufanya maamuzi ambayo ni maamuzi sahihi kuhusu udhibiti wa uchafu wa chanjo za COVID-19. 

"Katika kukabiliana na COVID-19, usimamizi endelevu wa taka za afya ni muhimu zaidi kuliko hapo awali ili kulinda jamii, wafanyikazi wa afya, na sayari na kuzuia uchafuzi wa mazingira," anasema Ruth Stringer, mratibu wa sayansi na sera kwa huduma ya afya bila madhara.