Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika inahitaji haraka dozi milioni 20 kwa ajili ya chanjo ya marudio ya COVID-19:WHO 

Muhudumu wa afya akitoa chanjodhidi ya COVID-19 nchini Sudan Kusini
© UNICEF/Bullen Cho Mayak
Muhudumu wa afya akitoa chanjodhidi ya COVID-19 nchini Sudan Kusini

Afrika inahitaji haraka dozi milioni 20 kwa ajili ya chanjo ya marudio ya COVID-19:WHO 

Afya

Afrika inahitaji angalau dozi milioni 20 za chanjo ya Oxford-AstraZeneca katika wiki sita zijazo ili kuwapa dozi za pili wote ambao walipata chanjo ya kwanza ndani ya muda wa wiki 8 - 12 kati ya kipimo kilichopendekezwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. 

WHO imesema dozi moja ya chanjo ya Oxford-AstraZeneca inatoa karibu asilimia 70% ya ulinzi kwa angalau wiki 12.  

Takwimu kuhusu kinga baada ya kupokea dozi ya kwanza ya chanjo baada ya wiki 12 ni ndogo, hata hivyo kingamwili za COVID-19 zimebainika mwilini hadi miezi 6 baada ya chanjo ya kwanza  limeongeza shirika hilo. 

Dozi kamili inayotolewa na muda wa wiki 12 baada ya dozi ya kwanza inatoa ulinzi wa asilimia 81% kwa muda mrefu. 

Muhudumu wa afya akimchanja mtu wa pili kupata chanjo ya COVID-19 nchini Angola kwa mfumo wa COVAX.
© UNICEF/COVAX/Carlos César
Muhudumu wa afya akimchanja mtu wa pili kupata chanjo ya COVID-19 nchini Angola kwa mfumo wa COVAX.

Watu wengi bado hawajapata chanjo 

 Mbali na hitaji hili la dharura, WHO inasema dozi zingine milioni 200 za chanjo yoyote ya COVID-19 iliyoorodheshwa na WHO kwa matumizi ya dharura inahitajika ili bara la Afrika liweze kuchanja asilimia 10% ya idadi ya watu wake ifikapo Septemba 2021.  

Hii inafuata wito uliotolewa wiki hii na mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus katika Baraza la Afya duniani, linaloendelea na kikao chake cha 74 akitaka  nchi zote wanachama kuunga mkono msukumo mkubwa wa chanjo. 

Hadi kufikia sasa, dozi milioni 28 za COVID-19, za chanjo tofauti, zimetolewa barani Afrika, ambako chanjo ambazo zimeshatolewa zinawakilisha chini ya dozi mbili kwa watu 100.  

Kwa mujibu wa shirika hilo la afya duniani duniano kote jumla ya dozi za chanjo ya COVID-19 bilioni 1.5 zimeshatolewa. 

Dkt. Matshidiso Moeti mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa WHO amesema  

"Wakati dozi zinamalizika, kugawana dozi hizo za chanjo ni suluhisho la dharura, muhimu na la muda mfupi kuhakikisha kuwa Waafrika walio katika hatari kubwa ya maambukizi ya COVID-19 wanapata ulinzi unaohitajika. Afrika inahitaji chanjo sasa. Ukimya wowote katika kampeni zetu za chanjo utasababisha maisha ya watu kupotea na kupoteza matumaini. ” 

Ameongeza kuwa "Ni mapema sana kusema ikiwa Afrika iko kwenye kilele cha wimbi la tatu la maambukizi. Lakini, tunajua kuwa idadi ya wagonjwa inaongezeka, na saa zinakimbia kwa hivyo tunatoa wito kwa nchi ambazo tayari zimeshapatia chanjo vikundi vyao vilivyo hatari ili kuharakisha ushiriki wa kugawana dozi ili kulinda kikamilifu watu walio katika mazingira magumu. " 

Chanjo dhidi ya COVID-19 ni msingi wa kukabili janga la corona
Unsplash/Ivan Diaz
Chanjo dhidi ya COVID-19 ni msingi wa kukabili janga la corona

Kushirikiana dozi za chanjo 

Ufaransa ni nchi ya kwanza kushiriki chanjo za COVID-19 kutoka kwa usambazaji wake wa ndani, ikitoa zaidi ya dozi 31,000 kwa Mauritania, na nyingine 74 400 ambazo ziko tayari kusambazwa .  

Ufaransa imeahidi kushiriki dozi nusu milioni zaidi na nchi sita za Kiafrika katika wiki chache zijazo.  

Jumuiya ya Muungano wa Ulaya na nchi wanachama wake wameahidi dozi zaidi ya milioni 100 kwa nchi zenye kipato cha chini ifikapo mwisho wa 2021. 

Marekani kwa upande wake imeahidi kushiriki kugawa dozi milioni 80 kwa nchi zenye kipato cha chini, na nchi zingine zenye kipato cha juu zimeelezea nia ya kushiriki kusaidia kugawa chanjo.  

Kuhamisha ahadi hizi ni zinatimizwa haraka ni muhimu na kituo cha usimamizi wa usawa wa chanjo COVAX ni nyenzo iliyothibitishwa ya usambazaji chanjo wa haraka. 

UNDP inafanya kampeni ya kuelimisha umma kuhusu COVID-19 katika mji mkuu Mogadishu
UNDP Somalia/Ali Adan Abdi
UNDP inafanya kampeni ya kuelimisha umma kuhusu COVID-19 katika mji mkuu Mogadishu

Chanjo zisizotumika wanapewa wanaozihitaji 

Nchi za Kiafrika ambazo haziwezi kutumia chanjo zao zote zinazishiriki katika kuwagawia wengine wanaozihitaji bafrani humo limesema shirika la WHO 

Wakati hii inazuia upotezaji wa chanjo, kusambaza tena chanjo ni cha gharama kubwa na nchi lazima zitoe chanjo zote zilizopatikana haraka iwezekanavyo.  

WHO inafanya kazi kwa karibu na nchi kuboresha utoaji wa chanjo kwa kuimarisha mikakati ya utoaji na kuongeza matumizi. 

Kwa ajili ya muda mrefu, Afrika ni lazima iongeze uwezo wake wa utengenezaji wa chanjo limesema shirika hilo.  

Hata hivyo limesisitiza kwamba  hakuna suluhisho la haraka na kuweka sera, michakato na ushirikiano unaotakiwa inaweza kuchukua miaka mingi. Kusamehewa kwa kuhusu hati miliki ni hatua muhimu ya kwanza lakini lazima ije pamoja na ushirikiano wa utaalam na teknolojia muhimu. 

Muhudumu wa afya akiwa ameishika chanjo ya COVID-19 katika hospitali mjini New Delhi, India.
© UNICEF/Sujay Reddy
Muhudumu wa afya akiwa ameishika chanjo ya COVID-19 katika hospitali mjini New Delhi, India.

Wanachama wa WHO waunga mkono azimio 

 Zaidi ya nchi wanachama 100 wa WHO, pamoja na nchi 54 za Kiafrika zinashirikiana kufadhili rasimu ya azimio inayoongozwa na Ethiopia ambayo inawasilishwa katika mkutano wa Baraza la Afya Duniani wiki hii.  

Azimio hilo linalenga kuimarisha uzalishaji wa ndani wa chanjo, kukuza uhamishaji wa teknolojia na uvumbuzi, na kuzingatia makubaliano juu ya vipengele vinavyohusiana na biashara ya haki miliki na haki miliki za mali kupitia lensi ya kukuza uzalishaji wa ndani. 

WHO inasaidia wchi wanachama wa Afrika kuweka msingi wa kujenga uwezo wa utengenezaji wa chanjo.  

Karibu nchi 40 za Kiafrika zilijiunga na mafunzo ya hivi karibuni ya WHO ili kujenga uwezo wa utengenezaji na WHO inafanya kazi na Muungano wa Afrika AU, kusaidia mpango wa utengenezaji wa madawa wa kwa ajili ya Afrika, kusaidia masomo yakinifu na uhamishaji wa teknolojia inayowezekana kwa ombi maalum, kubadilishana utaalam na kusaidia kuunda ushirikiano muhimu. 

Dk Moeti amezungumza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari hii leo uliowezeshwa na Kikundi cha APO.