Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres anasema Afrika ni ‘chanzo cha matumaini’ kwa dunia 

Mwanamke mkulima akiwa amesimama mbele ya magunia ya nafaka yaliyohifadhiwa katika ghala katika kituo cha biashara nchini Sierra Leone.
FAO/Sebastian Liste
Mwanamke mkulima akiwa amesimama mbele ya magunia ya nafaka yaliyohifadhiwa katika ghala katika kituo cha biashara nchini Sierra Leone.

Guterres anasema Afrika ni ‘chanzo cha matumaini’ kwa dunia 

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo Jumamosi kupitia hotuba yake kwa njia ya video, ameueleza Mkutano wa 35 wa wakuu wa nchi na serikali wa Muungano wa Afrika, AU unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia kuwa Afrika ni "chanzo cha matumaini" kwa ulimwengu, akitoa mifano ya Eneo Huria la Biashara la Bara la Afrika na Muongo wa Ushirikishwaji wa Kifedha na Kiuchumi kwa Wanawake wa Afrika. 

António Guterres pia amesema kwamba, kwa miaka 20 iliyopita, Muungano wa Afrika, AU "umesaidia kuleta matumaini haya kuwa hai, ili kuwezesha bara kufikia uwezo wake wa juu." 

Anawakilishwa katika mji mkuu wa Ethiopia, na Naibu Katibu Mkuu, Amina J. Mohammed. 

Ushirikiano 

Kwa mujibu wa Bw. Guterres, ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na AU "una nguvu zaidi kuliko hapo awali", huku Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya 2063 (mchoro wa Afrika wa bara lenye amani, jumuishi na ustawi zaidi) kama nguzo kuu. 

Katibu Mkuu amesema kuwa, "ukosefu wa haki umejikita sana katika mifumo ya kimataifa", lakini ni Waafrika "wanaolipa gharama kubwa zaidi." 

Aidha amekumka kwamba kiwango cha chanjo katika nchi zenye kipato cha juu ni mara saba zaidi ya Afrika na kusema kwamba "mfumo wa kifedha wa kimataifa uliofilisika umezitelekeza nchi za Kusini."