Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusijidanganye, wimbi la tatu la Covid-19 Afrika halijaisha kabisa - WHO

Dorica Zuze na mwanae akiwa katika kituo cha afya  nchini Malawi.
© UNFPA/Joseph Scott
Dorica Zuze na mwanae akiwa katika kituo cha afya nchini Malawi.

Tusijidanganye, wimbi la tatu la Covid-19 Afrika halijaisha kabisa - WHO

Afya

Baada ya wiki nane mfululizo za kuongezeka kwa kasi ya maambukizi, sasa maambukizi mapya ya  Covid-19 barani Afrika yamepungua kasi, Afrika Kusini ambayo ndiyo ilikuwa na idadi kubwa ya maambukizi ikishuhudia kushuka kwa kasi kwa maambukizi mapya ingawa maendeleo haya yanaweza kuwa ya muda mfupi, takwimu mpya kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO zimeonesha. 

Idadi ya maambukizi mapya barani Afrika imepungua kwa asilimia 1.7 hadi karibu watu 282, 000 katika wiki inayoishia Julai 18. Lakini ukiondoa takwimu za kutoka Afrika Kusini, ambayo inachangia asilimia 37 ya maambukizi haya, ambayo kimsingi kupungua kwake ndiko kunaonesha maambukizi kupungua, basi inaonekana kuna  kuongezeka kwa kipekee kwa maambukizi kwa wiki tisa. Kilele cha sasa ni asilimia 80 juu kuliko kilele cha awali cha Afrika bila takwimu kutoka Afrika Kusini.  

Dkt. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika amewasihi watu akisema, "usije ukajidanganya, wimbi la tatu la Afrika halijaisha kabisa. Hatua hii ndogo mbele inatoa matumaini na msukumo lakini haipaswi kufunika picha kubwa kwa Afrika. Nchi nyingi bado ziko katika hatari kubwa na wimbi la tatu la Afrika liliongezeka kwa kasi na juu zaidi kuliko hapo awali. Sherehe za Eid ambazo tumeadhimisha wiki hii pia zinaweza kusababisha kuongezeka kwa maambukizi. Lazima sote tuangalie mara mbili hatua za kuzuia ili kuimarisha hatua hizi dhaifu.” 

Nchi ishirini na moja za Kiafrika zimeshuhudia kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 20 kwa angalau wiki mbili mfululizo ambalo ni ongezeko la nchi tatu zaidi ya wiki iliyopita  na maambukizi mapya virusi vya corona aina mpya ya Delta ambayo imepatikana katika nchi 26 za Afrika. Aina nyingine ya Alpha iko katika nchi 38 na Beta iko katika nchi 35. Hatua iliyopigwa na Afrika Kusini bado haijulikani kwani maandamano yamevuruga mapambano ya nchi hiyo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, pamoja na ufuatiliaji wa magonjwa na upimaji. Mkusanyiko wa watu wenye vurugu pia unaweza kusababisha kuongezeka kwa visa. 

Hii inakuja wakati WHO inazihimiza nchi za Kiafrika kuongeza chanjo za coronavirus">COVID-19 haraka wakati kubana kwa usafirishaji wa chanjo kunapungua.