Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema katika ukanda wa Afrika, kifo 1 kati ya 5 vya COVID-19 vina uhusiano na ugonjw awa Kisukari.

Huduma ya bure ya ugonjwa wa kisukari yaokoa maisha ya vijana Kenya:WHO

WHO
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema katika ukanda wa Afrika, kifo 1 kati ya 5 vya COVID-19 vina uhusiano na ugonjw awa Kisukari.

Huduma ya bure ya ugonjwa wa kisukari yaokoa maisha ya vijana Kenya:WHO

Afya

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linasema huduma za bure za matitabu ya ugonjwa wa kisukari zimekuwa mkombozi mkubwa wa maisha hasa ya vijana wanaokabiliwa na ugonjwa huo nchini Kenya.

 

Miaka minne iliyopita Simon Maingi mwenye umri wa miaka 15 aligunduliwa kuugua ugonjwa wa kisukari, lakini ni baada ya kufanya safari kadhaa kwedna hospitalini.

Watoto wengine wanaokumbwa na hali kama hii, inayohitaji matibabu ya dawa ya insulini ya kila siku ili kuishi, hufariki kabla ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa huo kwa mujibu wa Zacharia Ndegwa Kariuki, mkuu wa mpango wa kitaifa wa kukabiliania na ugonjwa wa kisukari nchini Kenya.

Raghdad ambaye anaishi katika kambi ya wakimbizi nchini Jordan anaugua kisukari aina ya 1 na kila siku anatakiwa kujichoma insulini  lakini inamuwia vigumu kuhifadhi insulini hiyo katika hali ya baridi kutokana na joto kati ukosefu wa umeme
WHO/T. Habjouqa
Raghdad ambaye anaishi katika kambi ya wakimbizi nchini Jordan anaugua kisukari aina ya 1 na kila siku anatakiwa kujichoma insulini lakini inamuwia vigumu kuhifadhi insulini hiyo katika hali ya baridi kutokana na joto kati ukosefu wa umeme

 
Kwa Maingi, hatma ingekuwa tofauti bila ya huduma ya bure kutoka kwa kituo cha ugonjwa wa kisukari cha kibinafsi ambacho kimewasaidia zaidi ya watoto 3000 tangu kianzishe huduma zake za bure miaka 10 iliyopita. 

Ugunduzi uliochelewa au usiokuwepo na uhaba wa huduma ni kati ya changamoto kubwa zinazochangia hatua za kudhibiti ugonjwa wa kisukari. Wengi wa watoto wanaogunduliwa kuwa na kisukari ni kutoka familia maskini.  

“Hawawezi kumudu gharama ya matibabu”, kwa mujibu wa Dr Nancy Ngugi mwanachana kwenye bondi ya kituo kinachohusika na ugonjwa wa kisukari. 

Mwanzo wa matibubu ya ugonjwa wa kisukari ni kugunduliwa mapema. Ugonjwa wa kisukari wa aina ya 1 kwa sasa hauwezi kuzuiliwa.

Maingi anapata sindano za insulini kila siku na kufuatilia kiwango cha sukari kuweza kuudhibiti ugonjwa huo.

Mkazi huyu wa Ha Nam nchini Vietnam mwenye umri wa miaka 68 akionesha dawa zake za kutibu ugonjwa wa kisukari
© WHO/Quinn Mattingly
Mkazi huyu wa Ha Nam nchini Vietnam mwenye umri wa miaka 68 akionesha dawa zake za kutibu ugonjwa wa kisukari

Muriuki kutoka mpango wa kitaifa wa kuzuia ugonjwa wa kisukari anasema kati ya watoto 50,000 na elfu 70,000 wanaishi na ugonjwa wa kisukari aina ya 1. 

“Alikuwa anapoteza uzani, na kila mara alihisi njaa,” anakumbuka Dorcus Nthenya, mama yake Maingi, kabala ya mwanawe kugunduliwa.  
“Alikuwa na uchovu kila wakati angeweza hata kuzimia. Tulimpeleka hospitalini mara kadhaa. Hatukuelewa tatizo lilikuwa wapi.” 
 
Wakati mmoja wa wagonjwa wake hapati nafuu, shirika hilo lisilo la serikali linamtembelea nyumbani kuona ni uangalizi upi anahitaji na kutoa suluhu. 

Baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa wa kisukari, Maingi akawa mmoja wa watoto 3,000 waliosajailiwa kwenye kituo hicho katika mpango wa watoto unatoa huduma za bure, na kuwafuatilia wagonjwa hao. 

Visa vya ugonjwa wa kisukari vimekuwa vikiongezeka nchini Kenya kutokana na mabadiliko ya idadi ya watu na ya kijamii ikiwemo ukuaji wa miji, watu wanaozeeka na mifumo ya maisha isiyo zingatia afya kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2015 ambao pia uligundua kuwa asilimia 88 ya watu hawafahamu hali zao kuhusu ugonjwa wa kisukari. 

Afisa wa afya akifanya uchunguzi wa kisukari kwa mgonjwa barani Afrika.
WHO/Africa
Afisa wa afya akifanya uchunguzi wa kisukari kwa mgonjwa barani Afrika.

Mwaka 2018 wizara ya afya ilifanya ushirikiano na kituo kinachohusika na ugonjwa wa kisukari na mashirika mengine kuandaa miongozo ya kitaifa ya kutibu ugonjwa wa kisukari aina 1 na 2 na mtaala wa kuwafunza wahudumu wa afya kuhusu ugonjwa wa kisukari. 

Wilson Maina anakumbuka wakati bintiye mwennye umri wa miaka 10, Margaret alipogunduliwa kwa mara ya kwanza kuwa na kisukari.  
Bili ya dola 340 na dola 40 za dawa kila mwezi ilikuwa gharama kubwa kwake na hadi akafikia kiwango cha kushindwa kumudu karo yake. 

Kwa msaada kutoka kituo kinachohusika na ugonjwa wa kisukari, Maina anasema aliweza tena kumlipia mtoto wake karo, “Tumegundua kuwa watoto ambao wameandikishwa kwenye kituo hiki, afya zao zimeimarika, waliweza kuhitimu umri wa kubalehe, wakaendelea na masomo na matokeo yakawa mazuri shuleni,” Dr Ngugi anasema. 

Huduma ziliendelea na kuongezeka wakati wa janga la COVID-19. Wagonjwa waliosajiliwa kwenye kituo cha kutoa huduma kwa wagonjwa wa kisukari wanaendelea kupata madawa na huduma za bure. Programu hiyo pia imepanua wigo wa kuwahudumia wagonjwa hadi watakapotimia umri wa miaka 25.