Mabaharia ni wafanyakazi muhimu na wa msitari wa mbele wanaostahili kupewa haki:UN 

IMO yataka mabaharia wachukuliwe kama wafanyakazi muhimu wa msitari wa mbele
IMO
IMO yataka mabaharia wachukuliwe kama wafanyakazi muhimu wa msitari wa mbele

Mabaharia ni wafanyakazi muhimu na wa msitari wa mbele wanaostahili kupewa haki:UN 

Ukuaji wa Kiuchumi

Leo ni siku ya mabaharia duniani na katibu mkuu wa shirika la kimataifa la masuala ya bahari IMO Kitack Lim amesema mabaharia siku zote wamekuwa kitovu cha biashara duniani na kazi yao inagusa maisha ya kila mtu iwe ni chakula kinawekwa mezani kwetu, dawa zinazodumisha afya ya kila mtu, kompyuta zinazotumika kwa kazi au kujiburudisha au magari yanayotusafirisha kila siku. 

Amesema “vitu vyote hivyo husafirishwa na meli kupitia baharini, lakini janga la corona au COVID-19 limesababisha changamoto kubwa atika maisha ya kila siku kwa watu hawa ikiwa ni pamoja na ugumu wa fursa za kufikia bandari, usafirishaji, kubadilisha mabaharia waliokwama melini na mengine mengi.” 

Hivyo katika siku hii ametoa wito na kuzichagiza serikali kuwaunga mkono mabaharia ambao ni wafanyakazi muhimu na wa msitari wa mbele hasa katika wakati huu wa janga lakini pia kusambaza ujumbe unaotaka kuwe na mustakbali wenye haki kwa mabaharia. 

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii amesema dunia inategemea usafirishaji wa bahari na mabaharia, lakini maisha na kazi za mabaharia hao zimeathirika vibaya na na janga la COVID-19. 

Meli zikiwa katika bandari ya Antwerp
Picha/ IMO
Meli zikiwa katika bandari ya Antwerp

Ameongeza kuwa “Wakati wote wa shida, mabaharia wamekabiliwa na changamoto kubwa juu yakuweza kurejea nyumbani, kusafiri kujiunga na meli zao, upatikanaji sahihi wa chanjo na huduma za matibabu, na kuondoka pwani. Walakini mabaharia kwenye meli wameendelea kufanya kazi, wakitoa huduma muhimu kwa watu kila mahali.” 

 Ameongeza kuwa wafanyikazi hawa wa kimataifa ambao ni juumla ya watu milioni 1.6 lazima watambulike kama wafanyikazi muhimu wanaotoa huduma muhimu, na wapewe nafasi ya kusafiri na kurejea nyumbani.  

Mabaharia lazima pia wawe na fursa sawa ya ufikiaji wa chanjo, kwani hakuna mtu aliye salama mpaka kila mtu awe salama. 

Mwaka 2020 Guterres amesema, idadi ya mabaharia wanaohitaji kutolewa na kubadilishwa kutoka kwenye meli zilizokwama ilifikia kiwango cha juu cha mabaharia 400,000.  

UN inataka mabaharia na wahudumu wa ndege kuchukuliwa kama wahudumu wa msitari wa mbele na hivyo kupewa kipaumbele katika chanjo ya COVID-19
IMO/Hedi Marzougui
UN inataka mabaharia na wahudumu wa ndege kuchukuliwa kama wahudumu wa msitari wa mbele na hivyo kupewa kipaumbele katika chanjo ya COVID-19

Hata hivyo ameongeza kuwa “Shukrani kwa juhudi za pande zote zinazohusika, idadi hiyo kwa sasa imepungua na inakadiriwa kuwa karibu 200,000.” 

Lakini amesema ushuru kwa mabaharia unaendelea kuwa mkubwa. Lazima tufanye jitihada zaidi kusaidia wafanyikazi waliochoka na kusisitizwa umuhimu wa kuwasaidia ambao hufanya kazi katika meli zinazosafirisha bidhaa muhimu  ikiwa ni pamoja na chakula, mafuta na vifaa vya matibabu.  

Amesisitiza kuwa “Hili ni suala la kibinadamu na tusipofanya hivyo ni tishio linalowezekana kwa usalama wa usambazaji wa bidhaa muhimu.” 

Hivyo amesema katika siku hii ya mabaharia “Ni lazima tutambue kwamba mustakbali wa biashara ya dunia unategemea watu ambnao wanaendesha sekta ya meli na wadau wpote lazima wafanye kazi pamoja kuhakikisha mustakbali wenye usawa kwa mabaharia.”