Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Baharia akiwa ndani ya meli kwenye Bandari ya Felixstowe nchini Uingereza.

Dunia inawategemea sana mabaharia, lazima tuwathamini:Guterres

© IMO
Baharia akiwa ndani ya meli kwenye Bandari ya Felixstowe nchini Uingereza.

Dunia inawategemea sana mabaharia, lazima tuwathamini:Guterres

Ukuaji wa Kiuchumi

Mchango wa mabaharia haupimiki nani muhimu sana kwa watu na maendeleo yao, kwani dunia inawategemea sana amesem Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Kupitia ujumbe wake maalum wa siku ya mabaharia duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Juni 25 Katibu Mkuu amesema “Meli husafirisha asilimia 90 ya bidhaa za ulimwengu kuanzia nafaka na nishati, hadi bidhaa za watumiaji na mengi zaidi. Bila meli na wanawake na wanaume wanaofanyakazi katika meli hizo, uchumi ungedorora na watu wangekufa njaa.” Ameongeza kuwa mabaharia kote ulimwenguni wanakabiliwa na changamoto kubwa zinazotokana na janga la COVID-19 zikijumuisha kandarasi za kazi zilizoongezwa kwa muda mrefu zaidi ya tarehe zao za mwisho na vipindi virefu vya kutoa huduma,lakini pia changamoto zinazohusiana na chanjo, matibabu na likizo nje ya bahari. Maudhui ya siku ya mabaharia mwaka huu ni "Safari yako, awali na sasa" maudhui hayo ni fursa ya kutambua jukumu muhimu la mabaharia, na kutazama mustakbali wao. Guterres amesema zaidi ya yote, “Hii inamaanisha kuwasikiliza mabaharia wenyewe. Wanajua vizuri zaidi kuliko mtu yeyote mahitaji yao na kile ambacho tasnia hii inahitaji kufanya ili kushughulikia changamoto kuu zinazowakanbili. Hii ni pamoja na upanuzi wa huduma za hifadhi ya ulinzi wa jamii, mazingira bora ya kazi, kushughulikia tatizo la mabadiliko ya wafanyakazi, kutumia zana mpya za kidijitali ili kuimarisha usalama na ufanisi, na kufanya sekta hii kuwa inayojali mazingira na endelevu zaidi.” Katibu mkuu amehitimisha ujumbe wake akisema kwamba “Katika siku hii ya kimataifa ya mabaharia, tunarejea dhamira yetu ya kusaidia mabaharia kila mahali, na kuheshimu ujuzi, taaluma na uzoefu wanaoleta kwenye tasnia hii muhimu.” Wakati wa kutafakari mustakbali wa mabaharia NayeKatibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya bahari IMO Kitack Lim katika ujumbe wake wa siku hii amesema “Safari ya kila baharia ni tofauti, lakini wote wanakabiliwa na changamoto zinazofanana. Kwa mwaka wa 2022, kampeni ya siku ya mabaharia yenye kaulimbiu safari yako awali na sasa, shirikisha safari yako,inaangalia safari za mabaharia, zinajumuisha nini na zinabadilika vipi wakati hadi wakati na kile kinachosalia katika kitovu cha ukweli kuhusu mabaharia.” Ameongeza kuwa kampeni hii inawapa mabaharia nafasi ya kushiriki kile kinachowahusu kwa sasa, iwe ni tatizo la mabadiliko ya wafanyakazi ambalo halijatatuliwa au mustakabali wa teknolojia katika tasninia hiyo.