Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunahitaji kubadili mwelekeo ili kujikwamua na athari za COVID-19

Wafanyabiashara katika solo la Luanda angola, wamechukua hatua za kujilinda wakati wa janga la COVID-19
© FAO/ C. Marinheiro
Wafanyabiashara katika solo la Luanda angola, wamechukua hatua za kujilinda wakati wa janga la COVID-19

Tunahitaji kubadili mwelekeo ili kujikwamua na athari za COVID-19

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mabadiliko ya mwelekeo yanayolinganisha sekta binafsi na malengo ya kimataifa yahahitajika ili kushughulikia changamoto za siku za usoni, pamoja na zile zilizosababishwa na janga la corona au COVID-19, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hii leo Jumatatu, akihutubia kongamano la Ufadhili kwa ajili ya Maendeleo (FfD).

Katibu Mkuu António Guterres metoa taswira mbaya ya mwaka uliopita ambapo zaidi ya watu milioni tatu wamekufa kutokana na janga la COVID-19
Karibu watu wengine milioni 120 wametumbukia katika umaskini uliokithiri na ajira zipatazo milioni 255 zimepotea. Amebainisha kuwa kadiri kasi ya maambukizo inavyozidi kuongezeka, "janga hilo liko mbali zaidi kutokomezwa."

Msukumo mkubwa katika ngazi ya juu ya kisiasa unahitajika ili kubadili mwelekeo huu hatari, kuzuia wimbi lingine la maambukizi, kuepuka mdororo wa muda mrefu wa uchumi na kurudi kwenye kwelekeo unaotakiwa wa kutimiza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu na mkataba wa Paris wa 2015 wa mabadiliko ya tabianchi.


Mshikamano wa kimataifa katika mtihani

Kuendeleza mwitikio sawa wa kimataifa katika juhudi za kujimwamua kutoka kwa janga hilo la COVID-19 ni "kuuweka mshimakano wa kimataifa katika nchi nyingo kwenye mtihani wa majaribio " amesema mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa na "hadi sasa, tumeshindwa mtihani huo".
Ili kkufafanua hili Guterres, amesema kuwa nchi 10 tu ulimwenguni kote ndizo zinahodhi karibu asilimia 75 ya chanjo za COVID-19 zilizotolewa, akibainisha kuwa makadirio mengine yanaweka gharama ya dunia ya ufikiaji usio sawa na udhibiti wa chanjo kuwa ni zaidi yad ola trilioni 9.
Bwana Guterres alisisitiza haja ya " umoja na mshikamano ili kuokoa maisha na kuzuia zahma kubwa ya madeni na kutpokuwepo na utendaji."
Wito wa hatua muhimu
Ili kuweka msingi endelevu na wenye mnepo wah atua na mbinu za kujikwamua kutoka kwa janga la COVID-19 mkuu wa Umoja wa Mataifa  ametaka hatua za haraka zichukuliwe katika maeneo sita, zikianza na kuziba pengo la ufadhili wa mpango wa chanjo unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa, COVAX.
"Ili kumaliza kabisa janga hilo, tunahitaji ufikiaji sawa wa chanjo kwa kila mtu, kila mahali", amesema Katibu Mkuu. Pia ametaka msaada wa maendeleo, kwenda hasa mahali unakohitajika zaidi.


Suluhu na mzigo wa madeni

Mgogoro wa deni unahitaji kushughulikiwa vizuri, amesema Bwana Guterres ,ikiwa ni pamoja na kusitishwa kwa madeni, msaada, na ukwasi.
Amehimiza kuwa "Lakini tunahitaji kwenda mbali zaidi ya msamaha wa madeni, kwa kuimarisha mfumo wa kimataifa wa madeni ili kumaliza mizunguko mbaya ya wimbi la madeni, changamoto za kimataifa za madeni na miongo iliyopotea".
Kuwekeza katika mkataba mpya wa kijamii, unaotegemea mshikamano katika elimu, ajira zinazozingatia mazingira, ulinzi wa hifadhi ya jamii, na mifumo ya afyandio hatua ya tano ya kipaumbele cha mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambayo amesisitiza kuwa ni "msingi wa maendeleo endelevu na jumuishi".
"Jukwaa hili lazima litoe hamu na ari, kufadhili maisha ya baadaye, yenye umoja, yenye usawa na endelevu kwa wote", amehitimisha Katibu Mkuu.