Kufunga ndoa kwenye kambi ya wakimbizi haimanishi kutovaa shela la ndoto yako:Nour

16 Februari 2021

Kutana na mkimbizi Nour anayeishi kwenye kambi kubwa kabisa ya wakimbizi wa Syria ya Zaatari  nchini Jordan. Anamiliki duka la kushona na kuuza magauni ya harusi, kwani anaamini kwamba kufungia ndoa kambini sio tija ya bi harusi kutovaa gauni la ndoto yake katika siku hiyo muhimu maishani.

Katikati ya mtaa wa soko maarufu kama Shams Elysee kambini Za’atar maduka yamesheheni na moja wapo ni Nour saluni linalouza maguani ya harusi na kupamba maharusi na mmiliki wake kwa miaka mitatu sasa ni Nour mwenyewe “Wakati bwana harusi anapokuja dukani kumchukua bi harusi ni furaha kubwa na inanifurahisha zaidi kwamba wanapenda kazi yangu.” 

Katika kambi hii ya Zaatari iliyofunguliwa mwaka 2012 ambayo ni maskani ya wakimbizi 80,000 wa Syria wanahudumiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa, kuna maduka mengi katika mtaa huo wa soko lakini saluni ya Nour ni ya aina yake kwani mbali ya kushona magauni ya harusi pia anawatengeneza nywele na kuwapamba maharusi hao na anasema 

“Kazi hii nahisi ni Sanaa, endapo kazi hii inagusa moyo wako, basi unajua ni lazima uifanye.” 

Mona ambaye pia ni mimbizi kutoka Syria na bi harusi mtarajiwa na leo amefika dukani kwa Nour baada ya kuelekezwa sifa zake na ubora wa nguo na huduma zake,“Nimekuja kuchagua gauni la harusi, kwani nimehadithiwa kuhusu saluni ya Nour kwamba mgauni ni mazuri sana na anafanya kazi nzuri. Nadhani nitachagua gauni jekundu ni rangi ya wapendanao na mchumba wangu anapenda rangi nyekundu.” 

Pamoja na umaarufu wa duka lake janga la corona au COVID-19 limekuwa mwiba kwa Nour, kwani harusi zimepungua na theluthi moja ya wakimbizi nchini Jordan wamepoteza ajira,hata hivyo hali hiyo haijamkatisha tamaa kwani sasa badala ya kusubiri wateja kuja dukani anachukua vipodozi na magauni na kuwafuata majumbani kwao.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter