Mkimbizi kambini Za’atari Jordan aunda roboti ya kupambana na COVID-19:UNHCR

3 Agosti 2020

Mkimbizi kutoka Syria anayeishi katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari nchini Jordan ameunda roboti kwa kutumia vifaa vya plastiki vya LEGO ambayo inasaidia kupambana na ugonjwa wa corona au COVID-19 kambini hapo. 

Katika maabara ya ubunifu kwenye kambi ya wakimbizi ya Za’atari mkimbizi Marwan kutoka Syria akionyesha roboti aliyoiunda ambayo inatoa vitakasa mikono au sanitizer bila kugusa chupa "Tumetengeneza roboti hii ilikuchangia kama wakimbizi , tunataka kuwa sehemu ya vita dhidi ya corona"

Kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR nia ya wakimbizi hawa wabunifu ni kuzuia maambukizi ya corona na kuchangia katika juhudi za kimataifa za kudhibiti ugonjwa huo. 

Marwan anaongeza pia “Lengo la kutengeneza robiti hii ni kusaidia jamii inayotuhifadhi na wakimbizi ndani ya kambi ya Za’atari kalini ipatikane pia nje ya kambi” 

Roboti hiyo imeundwa ndani ya kambi ya Za’atari na Marwan akiwashirikisha wakimbizi wengine wanaosomea masuala ya roboti. Marwan anasema roboti hiyo iliyotengenezwa kwa vipande vya plastiki vya LEGO imewekewa kifaa kama ubongo na ina sensa ambayo inatambua mtu akiweka mikono kupokea vitakasa mkono na kwamba kifaa hicho kimewashangaza wengi “Hata watu wenye uzoefu wa masuala ya roboti wanatuuliza kuhusu muundo na program ya roboti hii. Na sisi kama binadamu, kama wakimbizi tunapaswa kusaidia na sasa tumetengeneza roboti nyingi zaidi.” 

Matumaini ya Marwan ni kwamba ubunifu wake utakuwa mwanzo wa ubunifu mwingine mkubwa zaidi ili kudhihirisha talanta za wakimbizi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud