Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumeshtushwa na kulaani kilichotekea leo Washington DC: UN

Makao makuu ya Marekani mjini Washington D.C
Unsplash/Louis Velazquez
Makao makuu ya Marekani mjini Washington D.C

Tumeshtushwa na kulaani kilichotekea leo Washington DC: UN

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na hali iliyoendelea leo mjini Washington DC nchini Marekani na kuwataka viongozi wa kisiasa kuwaasa wafuasi wao kujizuia na ghasia.

Msemaji wa Katibu Mkuu Stephane Dujarric akijibu swali kwenye mkutano na waandishi wa Habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa alipoulizwa kuhusu kauli ya Umoja wa Mataifa kufuatia mamia ya waandamanaji kuvamia jengo kuu la serikali na bunge la Congress amesema “Katibu Mkuu ameshtushwa san ana matukio yanayoendelea kwenye mji mkuu wa Marekani Washington DC leo Jumatano. Nas katika mazingira hayo ni muhimu kwamba viongozi wa kisiasa kuwasisitiza wafuasi wao haja ya kujizuia na machafuko ,lakini pia kuheshimu mchakato wa kidemokrasia na utawala wa sheria.”
Kwa mujibu wa duru za Habari maelfu ya wafuasi wa Rais wa chama tawala wameandama kuvamia jengo kuu mjini Washington DC kwenye bunge la Congress ambako wabunge walikuwa wanakutaka kuhesabu kura za wawakilishi wa majimbo 50 ambao kimsingi ndio wanaoamua nani awe rais , mfumo ambao kwa kawaida humchagua Rais ambaye amepata kura nyingi za wananchi katika majimbo yao japo wakati mwingine Rais anaweza kuwa amepatya kura nyingi za wananchi na akakosa urais kwa kupoteza kura za wawakilishi wa majimbo kama ilivyokuwa kwa mgombea wa uchaguzi iliopita Bi Hillary Clinton.
Katika vuvurugu hizo duru za Habari zinasema mwanamke mmoja miongoni mwa waandamanaji amepigwa risasi kifuani na kuuawa huku milio ya risasi ikisikika wakati polisi walipojaribu kuwatawanya waandamanaji hao.

Mtazamo wa jengo kuu mjini Washington DC
UN News/ Mikhail Baranyuk
Mtazamo wa jengo kuu mjini Washington DC


Tunalaani machafuko-IPU

Nao Muungano wa Mabunge duniani IPU na jumuiya ya mabunge wamelaani vikali machafuko na mashambulizi kwenye makao makuu ya Marekani yaliyofanywa na waandamanaji leo Jumatano Januari 6.
Katika taarifa yake IPU imesema “Demokrasia na wawakilishi wa watu nchini Marekani lazima viheshimiwe.”  Rais wa IPU Duarte Pacheco amesema “Nalaani vikali jaribio hili la kukiuka katiba na utulivu wa kidemokrasia nchini Marekani.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa IPU Martin Chungong amesema “Nimesitikishwa san ana taarifa za machafuko kwenye bunge la congress nchini Marekani, hii ni hali isiyokubalika n ani kushambulia demokrasia na wawakilishi wake.