Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya demokrasia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema demokrasia ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa taarifa, ushiriki katika ufanyaji maamuzi na uwajibikaji wa kuchukua hatua hasa wakati huu ambapo dunia inakabiliana na janga la corona au COVID-19.