Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imelifungua tena soko la wakulima Cox's Bazar baada ya kulifunga sababu ya COVID-19 

Wakimbizi warohingya bado wanaishi wilaya ya Cox's Bazar nchini Bangladesh miaka kadhaa tangu wakimbie nchi yao ya Mynamar
© UNFPA Bangladesh/Carly Learson
Wakimbizi warohingya bado wanaishi wilaya ya Cox's Bazar nchini Bangladesh miaka kadhaa tangu wakimbie nchi yao ya Mynamar

WFP imelifungua tena soko la wakulima Cox's Bazar baada ya kulifunga sababu ya COVID-19 

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP wiki hii limelifungua  tena soko kubwa la wakulima kwenye kambi ya wakimbizi wa Rohingya ya Cox’s Bazar nchini Bangladesh baada ya kulifunga kwa miezi kadhaa kufuatia mlipuko wa janga la corona au COVID-19. Soko hilo ambalo ni sehemu ya mradi wa WFP ni neema sio tu kwa wakimbizi bali pia jamii inayowahifadhi.

Hili ni soko la wakulima katikati ya kambi ya wakimbizi wa Rohingya ya Cox’s Bazar sasa maisha yamerejea kama kawaida baada ya miezi kadhaa ya kufungwa kwa soko hilo kupunguza hatari ya  coronavirus">COVID-19. 

Soko hili lilianzishwa na WFP kama sehemu ya miradi yake kwa lengo la kuhakikisha wakimbizi wa Rohingya wanapata chakula safi kutoka shambani kwa ajili ya lishe bora. 

Popy Barua ni mmoja wa wakulima wadogowadogo ambao ni wenyeji na ni mchuuzi mwenye meza kwenye soko hili, mumewe aliyekuwa dereva wa lori alipata ajali na sasa hawezi kuendesha lori tana lakini anamsaidia mkewe kuuza sokoni mbogamboga na matunda na popy anatumia bidhaa hizo pia kutengeneza achali inayopendwa sana na wateja  wenyeji na wakimbizi,“Naweza kutengeneza achali ya mizaituni, achali ya ukwaju  na achali ya matunda damu na lakini pia naweza kutengeza achali ya maembe. Na huu ni msimu wa majani ya Tok Pata hivyo natengeneza achali ya kutumia majani hayo pia” 

Katika achali hiyo anachanganya viungo vingine mbalimbali ikiwemo binzari, chumvi, pilipili na vitunguu swaumu na mboga zingine kutokana na msimu.

Nchini Bangladesh kuna misimu sita ya kilimo na kila msimu unakuwa na aina tofauti za matunda na mbogamboga na idadi kubwa ya wakulima ni wanawake. 

WFP imeamua kutoa mafunzo na mikopo kwa wanawake hao  ili waweze kuanzisha biashara zao kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kusaidia familia zao .

Wengi biashara wanayofanya ni ya kuuza sokoni kama Popy  na kwa wastani huwapa kipato cha had idola 45,000 kila mwezi wa kwanza wa kuanza kwa soko , Popy anasema,“Baada ya kujiunga na soko hili la wakulima tunafanya kila kitu wenyewe, tunalima mbogamboga, tunazivuna na kuziuza, na kwasababu tunazilima basi tunajilisha, kulisha watoto wetu na pia kupata lishe.” 

Kwa mujibu wa WFP mrdi huu wa soko la wakulima umebadili maisha ya wakazi wa Cox’s Bazar na kuleta faida kubwa sio tu kwa wakulima kama Popy lakini pia kwa wakimbizi na jamii zinazohifadhi wakimbizi hao.