Watoto 55,000 hatarini kwa mafuriko na maporomo Cox’s Bazaar: UNICEF

1 Mei 2018

Watoto 55,000 wanakadiriwa kuwa katika hatari kubwa ya mafuriko na maporomoko ya udongo kwenye makazi ya wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Japo msimu rasmi wa mvua na pepo za Munsoon haujaanza ,Kwa mujibu wa UNICEF mvua za awali zimeanza na kuleta athari kwenye makazi hayo ya Cox’s Bazaar eneo linalotambulikwa kwa kukumbwa na mafuriko kila mara.

Mvua hizo ambazo zimeanza kunyesha tarehe 27 zikiambataza na kimbunga , kufikia leo zimeshaathiri maelfu ya familia na wakimbizi Cox’s  Bazaar wengi wakiwa ni watoto walioonekana kupanda juu ya paa za plastiki za makazi hayo ili  kujaribu kuzuia upepo kuyaezua. Christopher Boulerac ni msemaji wa UNICEF Geneva

( SAUTI YA CHRISTOPHER BOULERAC)

Tunakadiria zaidi ya watu 100,000  wakiwemo watoto 55,000 , wako katika hatari  kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo, inawezekana idadi hiyo ikafika hata 200,000 kutegemeana na ukubwa wa mvua.”

Ameongeza kuwa ingawa msimu ramsi utaanza Juni hali hii inadhihirisha ni jinsi gani msimu huo utakavyokuwa na athari kwa maelfu ya wakimbizi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter