Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Ethiopia wanaripoti vizuizi vya kufikia usalama nchini Sudan wakati idadi inakaribia 50,000 

Mfanyakazi wa UNHCR akihakikisha wakimbizi wa Ethiopia walioko Hamdayet, Sudan wanapat maji.
© UNHCR/Olivier Jobard
Mfanyakazi wa UNHCR akihakikisha wakimbizi wa Ethiopia walioko Hamdayet, Sudan wanapat maji.

Wakimbizi wa Ethiopia wanaripoti vizuizi vya kufikia usalama nchini Sudan wakati idadi inakaribia 50,000 

Amani na Usalama

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR, kwa kushirikiana na serikali ya Sudan, linasema sasa limesajili wakimbizi takribani 10,000 wa Ethiopia ambao wamevuka mpaka mashariki mwa Sudan, na wengine wakiripoti kulazimika kukwepa vikundi vyenye silaha ili kuufikia usalama. 

Msemaji wa UNHCR, Babar Baloch amewaeleza wanahabari hii leo mjini Geneva Uswisi kuwa wakimbizi waliokwisha vuka wakiwa wanakaribia 50,000, watu wanaovuka hivi karibuni kutokea maeneo ya ndani zaidi ya Tigray wanafika wakiwa dhaifu na wamechoka, wengine wakiripoti wametumia wiki mbili wakikimbia ndani ya Ethiopia walipokuwa wakienda mpakani. 

UNHCR bado ina wasiwasi mkubwa kuhusy usalama na hali ya wakimbizi wa Eritrea huko Tigray ambao wamekwama kwenye mzozo na hawajapata huduma kwa zaidi ya mwezi mmoja. “Tunakubaliana na wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kuruhusu kufika Tigray bila vikwazo ili kuwafikia watu wenye uhitaji. 

Tangu tarehe 6 ya mwezi huu wa Desemba, idadi ya wakimbizi wanaokimbia mzozo unaoendelea katika mkoa wa kaskazini wa Tigray imekuwa ikipungua hadi chini ya 500 kwa siku. 

Babar Baloch amesema, “wametuambia matukio ya kutisha ya kusimamishwa na vikundi vyenye silaha na kuporwa mali zao. Wengi wametumia muda kujificha kwenye mashamba na vichaka ili kuepuka kuonekana. Bila kuwa na nafasi ya kufika ndani ya Ethiopia hatuwezi kuthibitisha ripoti hizi zenye kusikitisha.” ufikiaji nchini Ethiopia hatuwezi kuthibitisha ripoti hizi zinazosumbua.” 

Aidha Msemaji huyo wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa amesema UNHCR bado ina wasiwasi mkubwa kuhusu usalama na hali ya wakimbizi wa Eritrea huko Tigray ambao wamekwama kwenye mzozo na hawajapata huduma kwa zaidi ya mwezi mmoja. Na kwamba wanakubaliana na wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kuruhusu kufika Tigray bila vikwazo ili kuwafikia watu wenye uhitaji. 

“Tunarudia wito wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa pande zote kuruhusu uhuru wa kusafiri kwa raia walioathiriwa wanaotafuta msaada, usalama, na usalama ndani ya mkoa wa Tigray au nje ya maeneo yaliyoathiriwa. Hii ni pamoja na kuheshimu na kudumisha haki ya kuvuka mipaka ya kimataifa kutafuta hifadhi.” Amesema Baloch 

Ndani ya Sudan, UNHCR inafanya kazi na serikali za mitaa na wadau, na inaendelea kuongeza misaada yake ya kibinadamu kusaidia wakimbizi wa Ethiopia. 

UNHCR inasema imeona maombi yanayoongezeka ya kutafuta familia, kwani wengi walitenganishwa mwanzoni mwa mzozo au wakati wa kukimbia na hawajaweza kuwasiliana tangu wakati huo. Dawa zaidi zinahitajika, hasa kwa wale ambao walikuwa wakitumia dawa za magonjwa sugu kama kisukari, Virusi Vya UKIMWI, VVU na magonjwa mengine. 

Pia UNHCR na wadau wake wanahitaji msaada ili kuzuia milipuko ya COVID-19, pamoja na vituo zaidi vya kunawa mikono, vifaa vya kujikinga na kampeni zaidi za uelimishaji  wakati wakimbizi wanaendelea kuwa katika hali ya msongamano. 

Kuanzia juzi Jumatano tarehe 9 Desemba, ndege ya kwanza kati ya tano zilizokodishwa zilianza kuleta vifaa vya misaada ya kibinadamu vinavyohitajika haraka nchini Sudan. Kwa jumla, ndege kutoka Dubai na Nairobi zitaleta mahema 3,225, blanketi 75,000, mikeka ya kulala 45,000, taa za nishati ya jua 20,000, Vyandarua vya kuzuia mbu 17,000 na karatasi za plastiki 8,250. Pamoja na safari hizi za ndege, UNHCR imesafirisha kwa ndege, tani 440 za misaada ya kibinadamu tangu tarehe 27 Novemba. 

UNHCR pia inaendelea kuhamisha wakimbizi mbali na mpaka na wengine 14,000 wamehamia makazi ya wakimbizi ya Um Rakuba hadi kufikia sasa. 

UNHCR na washirika wake wametoa wito wa ombi la  kwa dola za kimarekani milioni 147 kugharamia mahitaji na kuunga mkono serikali ya Sudan, ambayo inaendelea kukaribisha na kuhifadhi wakimbizi.