Dunia ina fursa kupitia mshikamano wa kimataifa kujijenga vyema upya:Guterres 

15 Septemba 2020

Katika mkesha wa kuanza kwa kikao cha 75 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA75, Katibu Mkuu António Guterres ameainisha changamoto zinazoikabili dunia na suluhu zinazoweza kupatikana kutokana na ushirikiano wa kimataifa. 

Katika wakati huu ambapo dunia inakabiliwa na changamoto kubwa zisizo tarajiwa zikitokana na janga la corona au COVID-19, mabadiliko ya tabianchi na vitisho vingine, Katibu Mkuu anasema anaona fursa za kubadili mwelekeo kutoka kwenye kujitenga na kuingia katika malengo ya pamoja. 

Na kwa kupitisha mshikamano wa kimataifa Guterres anasema dunia inaweza kujijenga upya vyema na kuwa na mustakbali bora, salama, wenye mafanikio na endelevu kwa wote. 

Miaka 75 ya Umoja wa Mataifa na COVID-19 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na UN news amesema COVID-19 ni tatizo, lakini pia ni fursa kwa sababu “tunatakiwa kubadilika tunapaswa kubadilika katika mwwlekeo ulio sahihi. Wakati tunakusanya rasilimali kwa ajili ya kujijenga upya tunaweza kujijengwa kwa njia sahihii na dira yetu inapaswa kuwa agenda yam waka 2030 na malengo ya maendeleo endelevu.” 

Hatua za kimataifa dhidi ya COVID-19 

Ili kukabiliana nna janga la COVID -19  Guterres amesema “tunahitaji chanjo kwa ajili ya kila mtu , kila mahali na katika mazingira ambayo ni nafuu kwa kila mtu kumudu, kwa sababu tutakuwa salama tu endapo kila mtu yuko salama.” 

Majaribio ya kutengeneza chanjo dhidi ya virus vya corona ikiendelea katika taasisi ya Jenner ya Chuo Kikuu cha Oxford.
University of Oxford/John Cairns
Majaribio ya kutengeneza chanjo dhidi ya virus vya corona ikiendelea katika taasisi ya Jenner ya Chuo Kikuu cha Oxford.

 

Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa mustakabali bora 

Suala linguine mtambuka linaloitikisa dunia hivi sasa ni mabadiliko ya tabianchi Guterres alipoulizwa nini kifanyike kuushinda mtihani huu amesema “Tunahitaji kujizatiti kikamilifu hususani kwa wachafuzi wakubwa wa hali ya hewa, na kwa wote tunahitaji mabadiliko katika hatua kwenye nishati, kwenye kilimo, kwenye viwanda , katika usafiri na katika nyanja zote za maisha yetu. 

Maendeleo ya wanawake ni faida kwa wote 

Changamoto nyingine kubwa kwa dunia hivi sasa ni kutimiza usawa wa kijinsia katika nyaja mbalimbali kuanzia za kijamii, kisiasa, na hata kiuchumi na kuhakikisha wanawake na wasichana wanawezeshwa. Kwa mantiki hiyo Guterres amessitiza kwamba “Wanaume wanapaswa kuelewa kwamba ni kwa maslahi ya kila mtu sipo tu ya wanawake kuhakikisha kwamba kuna uwiano na usawa wa kijinsia kwa sababu kwa kuhakikisha hilo dunia itakuwa bora zaidi.” 

Tunakuwa na nguvu tunaposhikamana 

Suala la mshikamano wa kimataifa na ujumuishwaji wa vijana ni suala ambalo Katibu Mkuu analipigia upatu sana. Amesema dunia inawajibika kuhakikisha inakidhi matakwa ya vijana. 

"Ahadi hii ni muhimu kwa vijana kwa mawazo ya huduma za afya kwa wote, mawazo ya kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, ya kuwa na haki na uswa katika jamii zetu, vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, Nyanja zote hizi zinadhihirisha dhamira kwa vijana. Na hilo ndilo tumaini langu kubwa katika kuzingatia mustakabali wetu wa pamoja.” 

Amehimiza kwamba “Tunahitaji kuwekeza katika mahusiano ya kijamii ili kufanya kila jamii, za watu wa asili, za walio wachache, na kila jamii kujihisi kwamba utambulisho wao unaheshimika lkini pia ni sehemu ya jamii kwa ujumla.” 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kati) akiwa  kwenye picha ya pamoja na vijana wanaoshiriki mkutano wa mfumo wa UN kwenye makao makuu ya UN New York Marekani (12 Aprili 2019)
UN /Mark Garten
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kati) akiwa kwenye picha ya pamoja na vijana wanaoshiriki mkutano wa mfumo wa UN kwenye makao makuu ya UN New York Marekani (12 Aprili 2019)

 

Fursa ya kubadili historia 

 amesema kizazi hili kina fursa kubwa ya kubadili historia n a kuandika historia mpya endapo itadhamiria kufanya hivyo.  

“Hebu na tuhakikishe kwamba tunausitishaji uhasama dunia nzima. Hebu tuhakikishe kwamba tutakuwa na chanjo ambayo ni kwa faida ya umma wa dunia, chanjo ya watu. Na hebu tuhakikishe kwamba tunapojenga upya chumi zetu tunafanya hivyo kwa kufikia lengo la kutokuwa na hewa ukaa ifikapo mwaka 2050.” 

 

Maeneo ya vinamasi hufanya kama "godoro" la kufyonza  hewa ya ukaa kutoka hewani
Photo: UNEP GRID Arendal/Steven Lutz
Maeneo ya vinamasi hufanya kama "godoro" la kufyonza hewa ya ukaa kutoka hewani

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter