Skip to main content

Mmenikirimu nami nalipa fadhila kwa kuwashonea barakoa:Mkimbizi Hamidullah 

Paris, Ufaransa
© Eric Ganz
Paris, Ufaransa

Mmenikirimu nami nalipa fadhila kwa kuwashonea barakoa:Mkimbizi Hamidullah 

Wahamiaji na Wakimbizi

Kutana na mkimbizi Hamidullah mwenye umri wa miaka 23. Baada ya kukimbia machafuko Afghanistan na kupokelewa na kukirimiwa na Kijiji cha Pessat-Villeneuve nchini Ufaransa kwa msaada wa shirika la Umoja wa  sasa analipa fadhila kwa kuisaidia jamii inayomuhifadhi kupambana na janga la corona au COVID-19.

Katika Kijiji kidogo cha Pessat-Villeneuve mkimbizi huyu Hamidullah anasaidia mapambano dhidi ya COVID-19 nchini Ufaransa kwa kutumia ujuzi wake wa ufundi cherahani aliourithi toka kwa mama yake. 


Anashona barakoa na kuzigawa bure kijijini kwake, “ufundi cherahani ilikuwa ni biashara ya mama yangu namshukuru yeye na Mola kwa sasa ni yangu pia na ninaweza kusaidia kupambana na corona.”


Janga la corona lilipozuka changamoto kubwa kijijini kwake ilikuwa ni barakoa akakata shuri na kuamua kusaidia.

Hamidulla ameshona zaidi ya barakoa 1000 na kwa msaada wa mamlaka ya eneo hilo ameweza kuzigawa kwa Kijiji kizima.


Gérard Duboisni meya wa Pessat-Villeneuve anasema, “sio barakoa ya kawaida, ni barakoa iliyotengenezwa hapa Pessat-Villeneuve na mkimbizi tunayemuhifadhi, napenda kusema ni wageni wetu.”


Nchini Ufaransa Hamidullah amepata usalama na ulinzi na sasa analipa fadhila kwa kutengeneza barakoa ili kuilinda jamii inayomuhifadhi, “ili kuvishinda virusi hivi kwa pamoja tutahitaji kuheshimu kanuni za usafi na tunahitaji kufanya hivyo kwa pamoja.”


Ili kumshukuru Hamidullah kwa juhudi zake ofisi ya mji huo imemtunukia medali ya kuthamini mchango wa wakimbizi na kusema, “wakimbizi wanaifanya Ufaransa kuwa tajiri , tunawasaidia wakimbizi lakini pia mnaisaidia Ufaransa kwa mchango wenu.”