Utoaji chanjo ya COVID-19 barani Ulaya uko katika kasi isiyokubalika: WHO  

1 Aprili 2021

Utoaji wa chanjo za COVID-19 barani Ulaya unaenda kwa mwendo wa polepole usiokubalika wakati maambukizi mapya yakiongezeka katika makundi yote, hiyo ni kwa mujibu wa ofisi ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO kanda ya Ulaya ambayo inashughulikia nchi na himaya 53.   

Nchi nyingi zimeshuhudia kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona wiki iliyopita, na visa vipya milioni 1.6 na karibu vifo 24,000, imeripoti WHO.  

“Chanjo zinaonesha njia bora ya kuondoka katika janga hili. Sio tu zinafanya kazi, pia zina ufanisi mkubwa katika kuzuia maambukizi. Hata hivyo, utolewaji wa chanjo uko katika mwendo usikubalika.” Amesema  Dkt. Hans Kluge, Mkurugenzi wa WHO, kanda ya Ulaya. 

Wasiwasi unaongezeka 

Miongoni mwa maeneo ya ulimwengu, Ulaya ni ya pili kuathiriwa zaidi na COVID-19. Jumla ya vifo vinakaribia haraka milioni moja, na kesi maambukizi yanaelekea kuzidi milioni 45.  

Kwa mujibu wa ofisi hiyo ya WHO, maambukizi mapya yanaongezeka katika rika zote isipokuwa isipokuwa watu wenye umri wa wa miaka 80 na zaidi na hivyo,  "kuonesha dalili za mapema za athari za chanjo. 

"Wiki tano tu zilizopita, idadi ya kila wiki ya maambukizi mapya barani Ulaya ilikuwa imeshuka hadi chini ya milioni moja, lakini sasa hali ya kanda hiyo inatia wasiwasi zaidi kuliko tulivyoona katika miezi kadhaa.” Amesema  Dkt. Dorit Nitzan, Mkurugenzi wa Dharura wa Kikanda wa WHO. 

Ongeza uzalishaji 

Dkt. Kluge amesema mradi chanjo uchanjaji unabaki chini, hatua zinazoendelea za afya ya umma bado zitapaswa kutekelezwa kuziba ratiba zilizocheleweshwa. 

"Wacha niwe wazi, lazima tuongeze kasi ya mchakato kwa kuongeza kasi ya utengenezaji, kupunguza vizuizi vya kutoa chanjo, na kutumia kila tulichonacho katika hazina, sasa.” Ameseisitiza Dkt Kluge. 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter