Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima tupambane na ukatili wa kingono kwenye mizozo na wakati wa COVID-19:UN

Msichana wa miaka 10, ambaye alikuwa mwathiriwa wa dhuluma, amesimama mbele ya nyumba yao huko Maradi, Niger.
© UNICEF/Frank Dejong
Msichana wa miaka 10, ambaye alikuwa mwathiriwa wa dhuluma, amesimama mbele ya nyumba yao huko Maradi, Niger.

Lazima tupambane na ukatili wa kingono kwenye mizozo na wakati wa COVID-19:UN

Wanawake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezitaka nchi kupambana kwa kungu zote dhidi ya ukatili wa kingono kwenye mizozo na wakati huu wa janga la viruzi vya Corona au COVID-19.

Kupitia ujumbe wake maalum wa siku ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kingono katika mizozo Guterres amesema “Ukatili wa kingono bado unatumika kama mbinu ya kivita na Zaidi yah apo uko katika mifumo tofauti tofauti kuanzia ubakaji, ndoa za shuruti, na kulazimishwa kubeba miamba au kutoa mimba. Uhalifu hu una uhalifumwingine wa kingono unaotekelezwa wakati wa vita mara nyingi hauadhibiwi hususan sasa ambapo dunia inakabiliwa na janga la COVID-19.”

Ujumbe wake pia umesisitiza kwamba uhalifu huu wa kikatili ndio chakula cha vita na unatoa tishio kubwa kwa amani na usalama wa kimataifa.

Sasa ni wakati mgumu sana kwa waathirika

Katibu Mkuu ameongeza kuwa janga la COVID-19 linaghubika maeneo yenye mizozo kote duniani , kwa waathirika wa ukatili wa kingono hali ni ngumu Zaidi. Na ni vigumu kwao kuripoti ukatili huo , vituo na mahali pa kwenda kupata hudumu ya kwanza huenda vimefungwa .

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amepongeza kazi inayofanywa na wahudumu wa masuala ya kijamii ambao wanaendesha na kutoa msaada kwa waathirika wa ukatili wa kingono licha ya vikwazo vya sasa na kuarantini.

Guterres amesisitiza kuwa “Leo katika siku ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kingono kwenye mizozo, tunaonyesha mshikamano na manusura wa ukatili huu. Wajibu wetu ni kuuzuia na kuukomesha uhalifu huu, kuwawajibisha wanaoutekeleza na kupanua wigo wa msaada kwa waathirika wote “

Mwaka 2009 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuanzisha kazi ya mwakilishi maalum wa kupambana na ukatili wa kijinsia katika mizozo. Kwa karne kadhaa ubakaji na ukatili vimekuwa vikichukuliwa kuwa ni sehemu ya vita.

Kwa muongo mmoja uliopita suala hili likaanza kuchukuliwa kuwa sio jambo lisiloepukika bali ni mbinu za makusudi za kivita na kujumuishwa katika makosa mabaya zaidi ya ukiukwaji wa sharia za kimataifa.

Tushikamane kuwasaidia wanawake Somalia

Nako Somalia mwakilishi maalum na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo James Swan ametoa wito kwa viongozi wa Somalia, jamii na washirika wote kufanya kila linalowezekana kuongeza msaada na kuwasikiliza waathirika na manusura wa ukatili huo uliotokana na vita.

Pia ametoa wito kwa waatu wote Somalia kushikamana na walioathirika na ukatili huo na kuchukua hatua za kuukomesha.

Pia amewashukuru na kuwapongeza wale wanaochukua changamoto na kukabiliana na kazi za hatari za kuhakikisha wanazuia ukatili huu.

Kazi ya Usanii ya Noorulhuda Nadheer
Noorulhuda Nadheer
Kazi ya Usanii ya Noorulhuda Nadheer

 

Amesema kwa mwaka 2019 idadi ya visa vya ubakaji vilivyoripotiwa nchini Somalia vilikuwa 744 ambapo 241 kati ya visa hivyo vilithibitishwa  kama ukatili wa kingono katika mizozo ukiwalenga wanawake na wasichana  lakini amesisitiza kuwa hata hivyo asilimia kubwa ya manusura wa ukatili huo hawatoi ripoti  kutokana na hofu na unyanyapaa uliopo katika jamii na hivyo unasalia kuwa ni ukatili unaoripotiwa kwa kiasi kidogo sana.

Mkuu huyo wa UNSOM amesema nchini Somalia waathirika na manusra 3,000 wa ukatili wa kingono, na ukatili mwingine wa kijinsia ukiwemo wa kingono katika mizozo wamepokea msaada wa huduma za afya mwaka jana na wengine 5,700 walipewa msaada wa kisaikolojia.

Ukatili wa kingono katika mizozo husanbabisha majeraha yasiyopona kwa wat una unasalia kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu kwa waathirika.

Lakini pia ni jeraha kwa jamii nan chi nzima na halina nafasi katika Somalia ya sasa inayoibuka na kuendelea amesema Bwana Swan.