Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miezi mitatu tangu kutangazwa COVID-19 ni janga bado hatukati tamaa- WHO

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akitoa taarifa kuhusu mlipuko wa COVID-19 mjini Geneva
UN Photo/Eskinder Debebe)
Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akitoa taarifa kuhusu mlipuko wa COVID-19 mjini Geneva

Miezi mitatu tangu kutangazwa COVID-19 ni janga bado hatukati tamaa- WHO

Afya

Ikiwa leo ni miezi mitatu tangu shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, litangaze kuwa ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 ni dharura ya kiafya ya kimataifa, shirika hilo limesema katu halijakata tamaa na halitokata tamaa katika kuhakikisha virusi hivyo vinatokomezwa.

Ikiwa leo ni miezi mitatu tangu shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, litangaze kuwa ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 ni dharura ya kiafya ya kimataifa, shirika hilo limesema katu halijakata tamaa na halitokata tamaa katika kuhakikisha virusi hivyo vinatokomezwa.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus, akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Geneva, Uswisi amesema kuwa azma yao ya kuendelea kuhudumia wakati wa dunia kupitia sayansi, mshikamano na sululu inaendelea na zaidi ya yote kwa kuzingatia ubinadamu na heshima kwa watu na mataifa yote.

Amesema, “WHO inafanya kazi kutoa mikakati mahsusi, suluhu na vifaa dhidi ya virusi vya Corona kwa nchi ambazo zitahitaji katika wiki na miezi ijayo. Jambo moja ambalo naomba ni umoja katika ngazi ya kitaifa na mshikamano katika ngazi ya kimataifa. Sasa kuliko wakati wowote ule, binadamu wanapaswa kuwa kitu kimoja na kutokomeza virusi hivi.”

Dkt. Tedros amekumbusha kuwa virusi vya Corona madhara yake ni makubwa kuliko hata shambulio la kigaidi, “linaweza kuleta misukosuko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Lakini chaguo ni letu na chaguo lenyewe linapaswa kuwa umoja katika ngazi ya taifa na msihkamano katika ngazi ya kimataifa.”

Akizungumzia mwelekeo wa baadaye ili kuweza kutokomeza virusi vya Corona, Dkt. Michael Ryan, ambaye ni Mkurugenzi wa WHO akihusika na programu za dharura, ametolea mfano wa Sweden ambayo haikuweka sera dhibiti ya watu kuzuia watu kuchangamana lakini ina miundo ya kipekee iliyowezesha maisha kuendelea kama kawaida huku idadi ya maambukizi ikiwa ni ndogo.

“Sweden imeweka sera thabiti ya afya ya umma kuhusu umbali wa kuchangamana, kuhudumia wat una kulinda watu katika vituo vyake. Na vitu vingine vingi. Kile ambacho imefanya tofauti ni kwamba inategemea sana uhusiano wake na raia na uwzo na utayari wa wananchi kutekeleza sera hizo na kujichunga wao wenyewe,”  amesema Dkt. Ryan.

Ameongeza kuwa, “nadhani iwapo tunataka kufikia mfumo wa kawaida wa maisha, nadhani kwa njia nyingi muundo wa Sweden unawakilisha muundo ujao. Iwapo tunataka kurejea katika jamii isiyo na katazo la kuchangamana, basi jamii inapaswa kuchukua muundo wa muda wa kati au muda mrefu ambao kwao katazo la magusano na kuchangamana kijamii litadhibitiwa na jamii yenyewe kutokana na uwepo wa virusi. Tunapaswa kutambua kuwa virusi vipo na kama mtu mmoja mmoja au jamii na familia zifanye kila liwezekanalo kila siku kupunguza maambukizi ya virusi.”

Baadaye hii leo WHO itaitisha kikao chake cha kamati ya dharura kutathmini hali halisi tangu COVID-19 itangazwe kuwa ni dharura ya afya ya umma duniani.

Hadi hivi sasa jumla ya watu 208,112 wamefariki dunia ulimwenguni kote kutokana na virusi vya Corona ikiwa ni miongoini mwa wagonjwa zaidi ya 300,000 waliothibitishwa.

Bara la Ulaya linaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi, ikifuatiwa na Amerika, Mediteranea Mashariki, kisha Pasifiki Magharibi, Kusini-Mashariki mwa Asia na Afrika ndio yenye wagonjwa wachache zaidi.