Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udaktari ni wito na ukiwa wako huchoki:Dkt. Wambugu

Pichani iliyopigwa kutoka angani inaonyesha sehemu ya makazi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya
Picha/Siegfried Modola
Pichani iliyopigwa kutoka angani inaonyesha sehemu ya makazi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya

Udaktari ni wito na ukiwa wako huchoki:Dkt. Wambugu

Wahamiaji na Wakimbizi

Kazi ya udaktari kama ilivyo ya ukunga au uuguzi ni wito na wakati majanga kama hivi sasa la virusi vya corona au COVID-19 umuhimu wake unakuwa hauna kifani. Kutana na daktari ambaye pampja na wenzae wanafanya kila wawezalo kuwakinda wakimbizi kambini Kakuma Kenya dhidi ya janga hilo.

Huyo ni mmoja wa madaktari kambini Kakuma Dkt. Jesse Wambugu akisema anafanya kazi kama afisa msaidizi wa afya kwenye kambi hiyo inayohifadhi wakimbizi takribani 196,000.

Licha ya changamoto na kuhudumia wagonjwa wengi kila uchao Dkt. Wambugu nasema

“Kinachonihamasisha kwanza kabisa ni wahudumu wa afya hapa ambao wako mstari wa mbele. Wana fanyakazi usiku na mchana kuhakikisha vituo viko tayari kupokea wagonjwa wowote”

Ameongeza kuwa hata wakati wa janga hilo la corona na hatari zote linalokuja nazo wahudumu hao hawachoki kwani ni wito wao na wanaendelea kufanya kazi.

Ameonezakuwa njia moja ambayo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR inayoitumia kuelimisha kuhusu usafi hasa kunawa mikono kambini hapo ni kupitia kampeni katika radio za Kakuma.

“Kila siku na katika kila mkutano tunaangalia endapo hatua za kujikinga tunazochukua zinatosheleza , au zitaweza kupunguza kusambaa kwa maambukizi na kuweza kuokoa maisha

Kwa Dkt. Wambugu kinga ni bora kuliko kuponya na hivyo wanawashirikisha wakimbizi katika kampeni za kujikinga.

Licha ya juhudi hizo anasema kinachomtia hofu ni endapo wanauwezo wa kutosha kuweza kukabiliana na janga la afya ya umma kama COVID-19. 

Kwa mantiki hiyo anasema huu ni wakati wa kupewa msaada ili waweze kuimarisha mbinu za kujikinga na kuchukua hatua mapema wanapoanza kupata wagonjwa wa corona.