Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yarefusha muda wa amri ya kutotembea usiku, COVID-19

Watu wengi wamepoteza ajira kufuatia hatua zilizochukuliwa kuzuia kusambaa kwa COVID-19.
UN News/ John Kibego
Watu wengi wamepoteza ajira kufuatia hatua zilizochukuliwa kuzuia kusambaa kwa COVID-19.

Uganda yarefusha muda wa amri ya kutotembea usiku, COVID-19

Afya

Nchini Uganda, Raisi Yoweri Kaguta Museveni ametangaza kurefusha muda wa kutekeleza sheria ya kutotembea usiku, kubana mijumwiko, usafiri wa umma na ule wa magari binafsi kwa wiki tatu katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19.

Amri ya kutotembea usiku iliotangazwa kwa majuma mawili ilifika ukomo saa kumi na mbili na nusu za asubuhi hii leo. Lakini saa nane baadaye, rais amehutubia taifa na kusema kwamba kulegeza kamba wakati huu itakuwa sawa na kutoa mwanya kwa mambukizi zaidi na hivyo kutangaza kurefusha muda huo kwa majuma matatu.

 “Kutokana na mafanikio tuliopata na changamoto zilizosalia, serikali imeamua kuendelea agizo la watu kutotoka majumbani kwa siku 21 zaidi kuanzia tarehe 15 Aprili 2020 hadi 5 Mei.  Hii ni kwa ajili ya kutusaidia kujipa mwanyamuda zaidi wa kufuatilia hali kwa muda mrefu zaidi ili tupate ushidi dhidi ya virusi hivi au kufahamu jinis gani tunavyoweza kuelelea kukabiliana navyo”

Ameongeza kuwa hili linamaanisha kwamba maagizo yote ya kinga dhidi ya COVIDI-19 yaliotolwa na serikali yataendleea kutekelezwa hadi mwisho wa majuma hayo matatu. Kubana usafiri wa umma, taasisi za elimu na aina yoyote ya mijumwiko ni miongoni mwa maagizo yaliokuwa yafike ukomo tarehe ishirini mwezi huu.

Miongoni mwa maagizo yaliotolewa hivi karibuni ni pamoja na kusitisha shughuli za wahudumu wa pikipiki wajulikanao kama boda-boda za kusafirisha mzigo baada ya saa nane mchana na kubana usafiri wa magari binafsi.

Wanaotoa huduma muhimu kama wahudumu wa afya na waganga wa mifugo, mamlaka za maji na umeme na wanahabari ni miongoni mwa wale waliokubaliwa kuendelea na kazi zao.

Masoko ya chakula nayo yanaendelea  lakini kwa kuzingatia maagizo ya wiyara ya afya kuhusiana na virusi vya corona au COVID-19.

Kwa sasa idadi ya wagonjwa waliothibitishwa ni watu 54 wakiwemo 7 walioaagwa. Hao ni kati ya watu 5664 waliopimwa baada ya kuwekwa chini ya karantini wakiwemo 4,015 waliorejea kutoka ngambo na kutambuliwa kuwa washikiwa wakuu.