Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati wa kuziba pengo la usawa wa kijinsia na ubaguzi ni sasa: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia kwenye chuo kikuu cha New school jijini New york kuhusu wanawake na usawa wa kijinsia
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia kwenye chuo kikuu cha New school jijini New york kuhusu wanawake na usawa wa kijinsia

Wakati wa kuziba pengo la usawa wa kijinsia na ubaguzi ni sasa: Guterres

Wanawake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kutokuwepo na usawa wa kijinsia na ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana ni ukatili unaopaswa kushughulikiwa sasa na si wakati mwingine wowote.

Guterres ameyasema hayo hii leo katika hotuba yake kuhusu “wanawake na mamlaka” kwenye chuo kikuu cha New School mjini New York Marekani ambako alitunukiwa stashahada.

Guterres amesema hali halisi ni kwamba “kila mahali wanawake wako katika hali mbaya Zaidi ya wanaume kwasababu tu ni wanawake.Wanawake wahamiaji na wakimbizi, wale wenye ulemavu na wanawake kutoka jamii zakila aina za walio wachache wanakumbana na vikwazo vikubwa zaidi. Ubaguzi huu unatuathiri sote.”

Amesisitiza kwamba kama ilivyokuwa utumwa na ukoloni katika karne iliyopita pengo la usawa kwa wanawake linapaswa kutuabisha sopte katika karne ya 21, kwani amesema “sababu sio tu kwamba haukubaliki bali ni upumbavu. Ni kwa kupitia tu ushiriki ulio sawa wa wanawake ndio tutaweza kufaidika na tunaweza kufaidika na akili, uzoefu na ufahamu wa wanadamu wote.”

Balozi wa amani akizungumza na wanafunzi katika shule mjini Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , kuhusu kuchagiza amani na usawa wa kijinsia
MONUSCO/Dominique Cardinal
Balozi wa amani akizungumza na wanafunzi katika shule mjini Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , kuhusu kuchagiza amani na usawa wa kijinsia

 

Umuhimu wa ushirikiswahi wa wanawake

Mbele ya hadhira hiyo iliyosheheni waalimu na wanafunzi Katibu Mkuu amehimiza kwamba ushirikishwaji wa wanawake ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha utulivu, kusaidia kuzuia migogoro na kuchagiza maendeleo endelevu na maendeleo jumuishi, kwanu usawa wa kijinsia ni kigezo cha kuwa na dunia bora.

Amesema hili sio suala jipya akitolea mfano wa jinsi wanawake ambavyo wamekuwa wakipigania haki zao kwa miongo na kusema miaka 500 iliyopita Malkia Nzinga Mbandi wa Mbundu alipigana vita dhidi ya utawala wa kikoloni wa Kireno unalojulikana leo hii kama Angola. Pia mwanaharakati wa haki za wanawake Mary Wollstonecraft, ambaye aliandika  Uthibitisho wa Haki za Wanawake mnamo 1792, mara nyingi huonekana kama mwanaharakati wa wanawake wa nchi za Magharibi. Na miaka 60 baadaye Sojourner Truth aliwasilisha ombi kwa ajili ya haki za wanawake wakati akifanya kila awezalo kukomesha utumwa.

Mshini wa tuzo ya amani ya Nobel na mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa Malala Yousafzai (Kushoto) and Nadia Murad balozi mwema wa UNODC kwa ajili ya utu wa manusura wa usafirishaji haramu wa binadamu.
UN Photo/Mark Garten/Manuel Elias
Mshini wa tuzo ya amani ya Nobel na mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa Malala Yousafzai (Kushoto) and Nadia Murad balozi mwema wa UNODC kwa ajili ya utu wa manusura wa usafirishaji haramu wa binadamu.

Uwezo wa wanawake kuongoza.

Na katika karne ya 21 vuguvugu la haki za wanawake limeshika kasi amesema Guterres huku wanawake walioshikilia nyadhifa za ukuu wa nchi wakifuta shaka na shuku zote kuhusu uwezo wa wanawake wa kuongoza.

Na kwa kutia msisitizo Zaidi azimio la haki za binadamu limeainisha usawa katika haki za wanawake na wanaume na mkataba wa kutokomeza mifumo yote ya ubaguzi dhidi ya wanawake limeainisha mtazamo wa usawa wa kijinsia.

Akitoa mfano amesema leo hii wasichana kama Malala Yousafzai na Nadia Murad wamevunja miiko na vikwazo vyote na kuunda mfumo mpya wa uongozi.

Bado kuna mtihani mkubwa katika haki za wanawake

Katibu Mkuu amesema licha ya hatua zote hizo zilizopigwa bado hali ya haki za wanawake ni mbayá “Kutokuwepo na usawa na ubaguzi imekuwa ada kila mahali , hatua zimedorora kila mahali na katika baadhi ya sehemu zimebadilika na kuna msukumo mkubwa wa kuzirudisha nyuma haki za wanawake. Ukatili dhidi ya wanawake ikiwemo mauaji umefikia kiwango cha kutisha zaidi ya mwanamke mmoja kati ya watatu atakabiliana na ukatili wa aina fulani katika Maisha yake.”

Ameongeza kuwa ulinzi wa kisheria dhidi ya ubakaji na ukatili majumbani vimevyana kama kitu cha kawaida. Ubakaji ndani ya ndoa unaendelea kuhalalishwa katika nchi 34 , na haki za wanawake za afya ya uzazi ziko katika tishio kubwa kutoka kila upande.

Pia amesema wanawake viongozi na mashuhuri katika jamii wanakabiliwa na udhalilishwaji, vitisho na ukatili , mtandaoni na nje ya mtandao. Kwa mamilioni ya wanawake na wasichana kufuatiliwa kuhusu uhuru wao binafsi ni hali halisi ya kila siku. Kuanzia kwenye serikali hadi kwenye makampuni n ahata kwenye hafla za kuenziwa wanawake wanaenguliwa mezani. Sera za kuwakandamiza na kuwaadhibu wanawake zinarejea kwa kishindo amesema Guterres huku mijadala ya amani ikiendelea kuwatenga wanawake miaka 20 baada ya nchi zote kutoa ahadi ya kuwajumuisha. Na zama hizi za kidijitali zinaweza kufanya pengo hilo la usawa kupanuka zaidi.

Vijana wa kike na wa kiume wanashiriki kwenye programu za kuelimisha umma kuhusu madhara ya ukeketaji na wito unaotolewa juu ya utekelezaji wa lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalotaka usawa wa kijinsia.
Warren Bright/UNFPA Tanzania
Vijana wa kike na wa kiume wanashiriki kwenye programu za kuelimisha umma kuhusu madhara ya ukeketaji na wito unaotolewa juu ya utekelezaji wa lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalotaka usawa wa kijinsia.

Dunia bado imetawaliwa na mfumo dume.

Katibu Mkuu amesema usawa wa kijinsia kimsingi ni suala la utawala “tunaishi katika dunia iliyotawaliwa na mfumo dume na yenye utamaduyni unaodhibitiwa na wanaume na tumefanya hivyo kwa karne. Mfumo dume ni aina ya mfumo ulioanzxishwa kuhusu urithi kupitia wanaume na hadi sasa mfumo huu unaendelea kuathiri kila nyanja ya maisha yetu na wote tunabeba gharam zake.”

Mfumo huu unakandamiza uchumi, mfumo wa kisiasa na ushirikiano wetu amesema Bwana Guterres.

Amesisitiza kuwa pengo la usawa lililojificha na limejengeka ndani ya taasisi na mifumo ambayo inaendesha maisha yetu lakini inatoikana na mahitaji ya nusu tu ya watu wote na hiuli limesababisha pengo kubwa la takwimu duniani , mara nyingi wanawake hawahesabiwi na uzoefu wao haujumuiswi” na athari zake ziko katika kila upande kuanzia huduma za vyoo hadi kwenye safari za mabasi na wako katika hatari kubwa ya kupata ajali kwani mikanda ya usalama hata kwenye magari imewekwa kwa kuwatosha wanaume. Wanawake wako kwenye hatari ya kufa na shinikizo la damu kwani hata vifaa vya kupimia vilitengenezwa kwa minajili ya mahitaji ya wanaume.”

Ameongeza kuwa athari zilizosababishwa na mfumo dume na pengo la usawa unaenda ,mbali zaidi ya wanawake na wasichana, akinukuu alichoandika mwandishi wa vitabu Chimamanda Ngozi Adichie: “Uanaume ni ngome ngumu ndogo na tunawaweka wavulana humo. Tunauelezea uwezo wa wanaume katika njia ambazo zinakuja na gharama kubwa kwa wanaume wenyewe.”

Faida za usawa wa kijinsia

Usawa wa kijinsia una faida kubwa kwa uhusiano wa kibinafsi wa wanaume. Wanaume wanaoshiriki utunzaji na kutumia wakati mwingi na familia zao wanafuraha zaidi, na wana watoto wenye furaha zaidi.

Kwa kiwango kikubwa, kubadilisha usawa wa mamlaka ni muhimu, sio tu kama suala la haki za binadamu, maendeleo ya kibinafsi, afya na ustawi.

Ni muhimu kutatua shida zingine zinazo haribu na kuchafua kizazi chetu, kuanzia kutokuwepo kwa usawa na upatanishi hadi mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi.

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73 María Fernanda Espinosa Garcés (kushoto),akiwa katika picha ya pamoja na Kersti Kaljulaid Rais wa Estonia, Katrín Jakobsdóttir waziri mkuu wa Iceland na  Paula-Mae Weekes,Ras wa Trinidad and Tobago baada
Picha na UN/ Mark Garten
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73 María Fernanda Espinosa Garcés (kushoto),akiwa katika picha ya pamoja na Kersti Kaljulaid Rais wa Estonia, Katrín Jakobsdóttir waziri mkuu wa Iceland na Paula-Mae Weekes,Ras wa Trinidad and Tobago baada

Maeneo matano yatakayobadili dunia yetu

Guterres amesema kuna maeneo matano ambayo katika kufikia usawa wa kijinsia yataweza kubadilisha ulimwengu wetu.

Mosi, migogoro na vurugu. Kuna mstari ulionyooka kati ya dhuluma dhidi ya wanawake, ukandamizwaji wa raia na migogoro.

Mabilioni ya dola hutumika kila mwaka kwa ajili ya amani na usalama. Lakini tunapaswa kujiuliza: amani ya nani? Usalama wa nani?

Kinyume chake, amesema kuwashirikisha viongozi wanawake na watoa maamuzi katika upatanishi na michakato ya amani huchangia amani ya kudumu na endelevu.

Umoja wa Mataifa umejitolea kuwaweka wanawake katikati ya juhudi zetu za kuzuia migogoro, kulinda amani, juhudi za kuleta amani na upatanishi na kuongeza idadi ya walinda amani wanawake.

Pili, mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi ni dharura kubwa ambayo tunakabiliwa nayo ni matokeo ya maamuzi ambayo yalichukuliwa sana na wanaume, lakini yana athari kubwa kwa wanawake na wasichana.

Ukame na njaa inamaanisha wanawake wanafanya bidii kupata chakula na maji, wakati mafuriko, joto la kupindukia, dhoruba na mafuriko huua wanawake na wasichana zaidi kuliko wanaume na wavulana.

Wanawake na wasichana kwa muda mrefu wamekuwa viongozi na wanaharakati wa mazingira, kuanzia Wangari Maathai na Jane Goodall hadi harakati zingine lakini athari za usawa wa kijinsia katika mabadiliko ya tabianchi zinakwenda mbali zaidi zaidi. “Dharura tunayokabiliwa nayo ni matokeo ya maamuzi yaliyochukuliwa na wanaume lakini athari zake ni kubwa sana kwa wanawake na wasicha. Usawa wa kijinsia unajumuisha wanaume kuongeza juhudi na kuwajibika kwani ni muhimu sana endapo tunataka kuyashinda mabadiliko ya tabianchi.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake barani Afrika
Daniel Getachew/UN Photo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake barani Afrika

Sehemu ya tatu ambayo haki za wanawake na fursa sawa zinaweza kuleta mafanikio ni katika kujenga uchumi jumuishi. Ulimwenguni kote, wanawake bado wanapata senti 77  tu kwa kila dola moja wanayolipwa wanaume. Utafiti wa hivi karibuni wa Jukwaa la Uchumi Duniani unasema itachukua hadi mwaka 2255 kuziba pengo la kijinsia la malipo. Pengo la malipo ni moja ya sababu ya kwa nini asilimia 70 ya watu masikini duniani ni wanawake.

Nne, Katibu Mkuu amesema ni kutokuwepo uwiano wa kidijitali. Wanawake wanachukua asilimia 26 tu ya ya ajira katika Akili bandia (AI), na hili halishangazi kwamba algorithms nyingi zinapendelea wanaume.

Teknolojia ya kidijitali inaweza kuwa msukumo mkubwa wa kufanya mazuri. “Lakini nina wasiwasi sana na mfumo dume uliotawala katika fani ya kiteknolojia katika vyuo vikuu. Hadi pale wanawake watakapokuwa na jukumu sawa katika kuunda teknolojia za kidijitali, mchakato wa haki za wanawake ndio utaweza kubadilika.”

Tano na mwisho guterres amesema ni eneo la, uwakilishi wa kisiasa. Ushiriki wa wanawake katika mabunge kote ulimwenguni umeongezeka maradufu katika miaka 25 iliyopita. Lakini uwakilishi wa wanawake katika serikali sio juu ya "maswala ya wanawake tu" kama ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia au kuchagiza utunzaji wa watoto. Wanawake kwenye serikali huleta maendeleo ya kijamii na mabadiliko halisi katika maisha ya watu.

Ameongeza kuwa wanawake wana uwezekano mkubwa wa kutetea uwekezaji katika elimu na afya; na kuleta muafaka katika vyama na masuala ya kawaida.

Wasichana vigori wakiondoka shuleni kwenye mji wa Bol nchi Chad baada ya muda wa masomo
UN Photo/Eskinder Debebe)
Wasichana vigori wakiondoka shuleni kwenye mji wa Bol nchi Chad baada ya muda wa masomo

Usawa wa kijinsia ni chachu ya kutimiza SDGs

Katibu Mkuu amesisitiza kwamba ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs leo la Usawa wa kijinsia ni lengo lenye ufunguo wa kufanikisha malengo mengine 16.

Muongo wa kuchukua hatua unakusudia kubadilisha taasisi na muundo, kupanua wigo wa ujumuishaji na kuhakikisha uendelevu.

Kufuta sheria ambazo zinabagua wanawake na wasichana; kuongezeka kwa ulinzi dhidi ya dhuluma; kuziba pengo katika elimu ya wasichana na teknolojia ya kidijitali; na kumaliza pengo la malipo ya kijinsia ni baadhi tu ya maeneo tunayolenga kwani uongozi sawa wa wanawake na ushiriki ni muhimu.

Tweet URL

 

Ukweli ulio bayana

Katibu Mkuu ameainisha bayana kwamba wanawake wamefanya mengi sawa na wanaume  na hata zaidi katika kila nyanja. Hivyo” Ni wakati wa kuacha kujaribu kubadilisha wanawake, na kuanza kubadilisha mifumo inayowazuia wanawake kufikia uwezo wao.”

Amesema miundo yetu ya mamlaka imekuwa ikibadilika pole pole kwa maelfu ya miaka. Lakini geuzi moja limengoja kwa muda mrefu. “Karne ya 21 lazima iwe karne ya usawa kwa wanawake. Hebu wote tutimize wajibu wetu katika kuifanya iwe hivyo.”