Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malizeni ubaguzi dhidi ya wanawake na watoto walioathiriwa na ukoma

Mhudumu wa afya akitembelea jamii nchini Brazil ili kukuza uelewa kuhusu kuzuia na kudhibiti ukoma
PAHO
Mhudumu wa afya akitembelea jamii nchini Brazil ili kukuza uelewa kuhusu kuzuia na kudhibiti ukoma

Malizeni ubaguzi dhidi ya wanawake na watoto walioathiriwa na ukoma

Afya

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya ugonjwa wa ukoma, mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu kutokomeza ubaguzi dhidi wa watu walioathirika na ukoma, jumapili ya leo ametoa wito kwa serikali kote duniani kumaliza ubaguzi rasmi na usio rasmi dhidi ya maeldu ya wanawake na watoto walioathirika na ukoma.

“Wanawake wengi na watoto walioathirika na ukoma ambao pia unafahamika kama ugonjwa wa Hansen ni waathirika wa unyanyapaa, unyanyasaji wa kimwili na kwa maneno, kucheleweshewa vipimo vya utambuzi na pia ukosefu wa uangalizi unaofaa.” Amesisitiza Bi Alice Cruz.

Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasiwasi wake kuhusu “kutokuwepo kabisa mipango maalumu ya mataifa kushughulikia mahitaji fulani ya wanawake na watoto walioathirika na ukoma na pia kutokomeza ubaguzi na vurugu dhidi yao.”

Ripoti ya mwisho ya Bi Cruz ilieleza kuwa visa vingi vya wanawake na watoto walioathirika, vinapita tu bila kuripotiwa.

Tweet URL

 

Maelezo ya Bi Cruz yanasema kuwa ingawa mifumo ya kinga ya watoto inaonekana kuathiriwa zaidi na ukoma, asilimia 10 hadi 20 ya watoto wanaacha kutumia dawa kwa kuwa matibabu yaliyopo hayafai kwa umri wao.

Zaidi ni kuwa wanawake walioathirika wanajikuta na msongo wa mawazo na hata mawazo ya kujiua hivyo mtaalamu huyo akatoa wito kwa serikali kote duniani kupata utatuzi kuhusu tatizo hili la ubaguzi.