Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna matumaini ya kasi mpya katika kupambana na ukoma, lakini unyanyapaa unaendelea. 

Mtu mwenye ukoma, Addis Abba, Ethiopia, April 2002
ILO/Fiorente A.
Mtu mwenye ukoma, Addis Abba, Ethiopia, April 2002

Kuna matumaini ya kasi mpya katika kupambana na ukoma, lakini unyanyapaa unaendelea. 

Afya

Ikiwa leo ni siku ya ukoma ulimwenguni, wataalam wanataka kukomeshwa kwa ubaguzi na unyanyapaa unaoendelea dhidi ya watu wenye ugonjwa huo. 

Wataalamu wanadai pamoja na maendeleo yanayofanywa katika vita dhidi ya ukoma, lakini mamilioni bado wanaathiriwa na ugonjwa huo, na wagonjwa wengi wanakabiliwa na kutengwa na jamii.  

Mtaalamu huru wa haki wa Umoja wa Mataifa,Alice Cruz amesema, “tunapaswa kujifunza kutokana na historia ya ukoma. Ili kupambana vyema na majanga, lazima tuondoe ubaguzi na upendeleo kwa wale ambao wameachwa nyuma.” Alice Cruz pia ni Mwakilishi huru katika kuondoa ubaguzi dhidi ya watu walioathiriwa na ukoma pamoja na familia zao. 

COVID-19 imetukumusha 

Bi Cruz anabainisha kuwa matokeo ya janga la COVID-19 - ambayo ni pamoja na kunyimwa haki ya kupata elimu, makazi na ajira, unyanyasaji wa majumbani na kijinsia, yanaonesha yale yanayowakuta wanaougua ukoma (pia hujulikana kama ugonjwa wa Hansen) kwa maelfu ya miaka. 

Mnamo Mei 2020, Mtaalam huyo huru wa Umoja wa Mataifa alitahadharisha kuhusu athari kubwa ambazo janga na virusi vya corona linasababisha kwa wanaougua ukoma, katika barua ya wazi iliyoelekezwa kwa serikali ambazo alitaka ziweke mipango ya kina ya hatua. 

Katika ujumbe wake kwa Siku ya leo ya Ukoma Ulimwenguni, Bi Cruz ameonya kuwa jibu lisilo la kutosha kutoka kwa nchi ambazo ugonjwa huo umeenea, huenda likasababisha kuzorota kwa udhibiti wa ukoma, uambukizaji na uzuiaji wa ulemavu, na pia kuzidi kwa hali mbaya sana ambayo tayari ipo.  

Kubadilisha mtazamo 

Ukoma unatibika, ikiwa matibabu yatafuata utambuzi wa haraka, lakini ikiwa wagonjwa hawatatibiwa, wanaweza kuachwa na tatizo la mwili na ulemavu ambao haurekebishiki.  

Hata hivyo, katika ujumbe wa siku ya leo wa Yohei Sasakawa, Balozi mwema wa utokomezaji wa ukoma, wa  shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO,  Yohei Sasakawa, anasema kuwa utambuzi wa mapema wa ukoma na matibabu ya haraka hayatoshi kushinda ugonjwa huo. 

"Inahitaji pia kubadilisha mawazo", anasema, Sasakawa akiongeza kuwa, "ili ukoma usiwe sababu ya aibu au upendeleo, lazima tuondoe vizuizi vyote kwenye njia ya wale wanaotafuta huduma ya matibabu. Lazima tuondoe vizuizi vinavyozuia watu walioathirika na familia zao kuishi kwa heshima na kufurahia haki zao za msingi za binadamu kama wanajamii kamili.” 

Bwana Sasakawa ameeleza imani kwamba mkakati wa ulimwengu wa ukoma wa mwaka 2021-2030 utaleta kasi mpya katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, na anatarajia, "jamii inayojumuisha ambayo kila mtu anaweza kupata matibabu na huduma bora, na kugunduliwa kwa ukoma na haiji tena na uwezekano wa athari mbaya za mwili, kijamii, kiuchumi au kisaikolojia ”.