Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni lazima kushughulikia changamoto 4 za karne ya 21 kwa suluhu 4 za karne ya 21:Guterres

Katibu Mkuu wa UN António Guterres (kushoto) akihutubia Baraza Kuu la UN kuhusu vipaumbele vyake kwa mwaka 2020 na mpango wa kazi wa shirika hilo.
UN /Mark Garten
Katibu Mkuu wa UN António Guterres (kushoto) akihutubia Baraza Kuu la UN kuhusu vipaumbele vyake kwa mwaka 2020 na mpango wa kazi wa shirika hilo.

Ni lazima kushughulikia changamoto 4 za karne ya 21 kwa suluhu 4 za karne ya 21:Guterres

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuna changamoto na dharura kubwa nne zinazotishia maendeleo yaliyopigwa katika karne ya 21 ambazo zinapaswa kushughulikiwa haraka. 

Akizungumza na nchi wanachama kwenye Baraza kuu hii leo mjini New York Marekani kuhusu vipaumbele vya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2020 na uzinduzi rasmi wa muongo wa hatua kwa ajili ya kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs, Guterres ametaja dharura hizo ambazo zinahitaji kipaumbele cha juu .

Changamoto kuu nne

Mosi ni, mivutano mkubwa zaidi wa ulimwengu katika miaka mingi, migogoro, ugaidi, hatari ya nyuklia, watu kulazimishwa kuhama makazi yao, na hatari ya mipasuko zaidi.  Amesema vita vinaendelea kusababisha madhila kila kona ya dunia. Mashambulizi ya kigaidi yanafanyika bila huruma na watu wanakimbia makwao kutokana na vita na mateso sasa kuliko wakati mwingine wowote tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Lakini pia mivutano ya kibiashara na teknolojia bado havijapatiwa suluhu.

Mtazamo wa Ziwa Tanganyika upande wa Tanzania ambalo ukubwa wake umepungua kwa sababu mbali mbali ikiwemo shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabianchi.
UN News/Assumpta Massoi
Mtazamo wa Ziwa Tanganyika upande wa Tanzania ambalo ukubwa wake umepungua kwa sababu mbali mbali ikiwemo shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabianchi.

Mgogoro wa tabianchi

Pili, uwezekano wa mgogoro wa hali ya hewa, muongo wenye joto zaidi katika historia, viumbe milioni moja viko hatarini kutoweka, dunia yetu inawaka.” Tunakabiliwa na zahma kubwa ya mabadilio ya tabianchi amesema Katibu Mkuu  na wansayansi wanasema ongezezko la joto baharíni hivi sasa ni la kasi kukoko wakati mwingine wowote. Katika mkutano ujao wa COP26 mjini Glasgow serikali lazima zilete mabadiliko ambayo yanahitajika duniani  na ambayo watu wanayataka kwa dhamira kubwa zaidi ya kukabili, kujenga ,nepo na kufadhili vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Ameongeza kuwa wajibu mkubwa uko kwa wachafuzi wakubwa . Nchi ambazo zinachangia pakubwa kwenye uchafuzi lazima zishike usukani kwenye vita hivi na zisipofanya hivyo basi “tumeangamia”. Guterres amesema “Bado ninaamini kwamba mabadiliko ya tabianchi ni vita ambavyo tunaweza kuvishinda. Wanasayansi wanatueleza kwamba bado hatujachelewa , huku wachumi na mameneja wakitujuza kwamba uwekezaji unaojali mazingira ndio ufunguo wa mashindano na kushinda changamoto hizo za karne ya 21. Umewadia wakati wa kupinga matumiazi ya mara moja ya bidhaa za plastiki.

Maandamano nchini Lebabon
Jamil Karam
Maandamano nchini Lebabon

Kutoaminiana/ muongo wa hatua

Tatu, kutoaminiana kwa ulimwengu: watu wanashawishika kwamba utandawazi haufanyi kazi kwao, kushuka kwa imani katika taasisi za kisiasa.  Kama moja ya ripoti zetu ilivyodhihirisha jana, watu wawili kati ya watatu wanaishi katika nchi ambazo pengo la usawa limeongezeka. Usifanye makosa katika dunia ya sasa ongezeko la pengo la usawa linazamisha mashua zote.

Guterres amesema anashuhudia hamasa ya malengo ya maendceleo endelevu kila kona anayokwenda kuanzia kwa viongozi wa kisiasa katika ngazi ya kitaifa hadi mashinani, kwa wajasiriamali, wawekezaji, asasi za kiraia na wengine wengi.” Tunashuhudia hatua kubwa zinazopigwa kuanzia fursa za kupata huduma za afya ya uzazi hadi kwenye ongezeko la wanaoweza kutumia mtandao wa intaneti. Lakini tunachokishuhudia hakitoshi.”

Kwa sababu zote hizo tunazindua muongo wa utekelezaji wa maelengo ya maendeleo endelevu ifikapo 2030. Na kongamano la kwanza la hatua za SDG litakalofanyika Septemba litaainisha mchakato na kuweka mikakati ya mafanikio. Hivyo hebu na tuufanye mwaka 2020 kuwa muongo wa hatua na hebu tuufanye mwaka 2020 kuwa mwaka wa uharaka.

Natoa wito kwa nchi zote wanachama “wasikilizeni watu wenu, fungueni milango yote kwa wote kuweza kusikilizwa na tafuteni utangamano. Heshimuni uhuru wa kukusanyika kwa amani na kujieleza na lindeni maeneo ya umma na uhuru wa vyombo vya Habari.”

Nne, athari mbaya za ulimwengu wa dijitali: athari kwenye soko la ajira, kuenea kwa hotuba za chuki, Akili bandia AI hutoa uwezekano wa vitosho kama vile umiliki wa silaha hatari.

Roboti aliyepatiwa jina la Sophia ni miongoni mwa  ubunifu wa hali ya juu kwenye akili bandia.
UN /Manuel Elias
Roboti aliyepatiwa jina la Sophia ni miongoni mwa ubunifu wa hali ya juu kwenye akili bandia.

Nini kifanyike kushughilikia changamoto hizi

Katibu Mkuu amesema changamoto hizo kuu nne za karne ya 21  lazima zishughulikiwe na suluhu nne za karne ya 21 ambazo ni Mosi mtazamo wa amani na usalama kuzuia, kupatanisha, operesheni za ulinzi wa amani, kudumisha amani kunapelekea maendeleo ya muda mrefu.

Amesema anatiwa hofu kubwa na njia tofauti ambazo zinamomonyoa hali ya kuheshimu haki za binadamu duniani na ndio maana mwezi ujao mjini Geneva Uswis “nitazindua wito kwa ajili ya kuongeza hatua za kimataifa kuhusu haki za binadamu na utu wa binadamu.”

Pili amesema dhamira ya kukabiliana , kujenga mnepo na kufadhili mabadiliko ya tabianchi amesema tuko katika vita na asili ambayo inapambana vijkali. Na hatua za polepole hazisaidii tena hivyo wachafuzi wakubwa wachukue hatua zaidi Glasgow kwenye COP 26.

Tatu amesema lazima kuwe na usawa katika utandawazi kuchukua hatua kupitia muongo wa hatua za kutimiza malengo ya maendeleo endelevu .

Teknolojia

Na nne amesema kuchagiza teknolojia kwa mabadiliko chanya, kupambana na uhalifu wa mtandaoni na chuki mtandaoni, na kupiga marufumu kuhodhi silaha za mauaji .

Amesema utumiaji wa teknolojia utachukua nafasi za mamilioni ya ajira za watu ifikapo mwaka 2030 hivyo “tunahitaji kufanyia marekebisho mifumo yetu ya elimu, sio tu kusoma bali kusoma jinsi ya kujifunza katika maisha yetu. Na pia amesisitiza umuhimu wa kupambana na ugaidi, ubaguzi wa kuona weupe ni bora kuliko wengine na ubaguzi wengine ambao hupanda mbegu za chuki kwenye intaneti na mitandao ya kijamii. Ameongeza kuwa uhalifu mtandaoni unagharimu dola trilioni 6 kila mwaka. “Tunapaswa kushirikiana dhidi ya mgawanyiko wa kidijitali kwa kuchagiza ushirikiano wa kimataifa wa kidijitali”.

Wawezeshaji wa kushughilikia changamoto

Katibu Mkuu wa UN António Guterres (wa 2 kutoka kulia mstari wa mbele) akiwa na wanawake viongozi walio kwenye jopo la viongozi waandamizi kabisa wa UN, hatua ambayo inadhihirisha kauli yake ya kutekeleza usawa wa jinsia kwa vitendo.
UN /Mark Garten
Katibu Mkuu wa UN António Guterres (wa 2 kutoka kulia mstari wa mbele) akiwa na wanawake viongozi walio kwenye jopo la viongozi waandamizi kabisa wa UN, hatua ambayo inadhihirisha kauli yake ya kutekeleza usawa wa jinsia kwa vitendo.

Amesisitiza kuwa wawezeshaji wa yote haya ni haki za binadamu, , usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa vijana na mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa. Amekumbusha kuwa mwaka huu Umoja wa Mataifa unatimiza miaka 75 . akisema maadhimisho sio kusherehekea akimtaka kila mmoja kushiriki katika mjadala na kusema kwa pamoja tuiweke dunia katika mstari wa kuhakikisha inaleta mabadiliko.

Mabadiliko kwenye UN

Guterres amesema kuanzia siku ya kwanza na kwa ushirikiano w anchi wanachama amekuwa akifanya mabadiliko mbalimbali ikiwemo kutoa fursa, uwazi na uwajibikaji.

Mwaka 2020 ameahidi kuendeleza mafanikio hayo amesema “tumeanza mwaka huu kwa mafanikio makubwa kwani Januari mosi kwa mara ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa tumefikia usawa wa kijinsia katika nafasi za ngazi ya juu za kazi za Umoja wa Mataifa kwa wanaofanya kwazi wakati wote  hasa ngazi ya wasaidizi wa Katibu Mkuu. Tumetimiza hilo kwa miaka miwili kabla ya muda tuliopanga.”