Vita dhidi ya uchafuzi wa bahari ni zaidi ya kukomesha plastiki:Guterres

9 Juni 2018

Kulinda bahari dhidi ya uchafuzi ni kunahitaji juhudi zaidi za pamoja na sio kupambana na plastiki pekee ni kuchukua kila hatua inayohitajika kuhakikisha changamoto zote za bahari zinashughulikiwa , pongezi kundi la G-7 kwa kuchukua hatua leo, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akuzungumza kwenye mkutano wa 44 wa kundi la G-7 La Malbaie huko Quebec nchini Canada, ambako amekaribisha uamuzi wa kundi hilo kutoa kipaumbele katika sual la bahari “Nakaribisha mkataba wa leo wa plastiki uliopitishwa na G , lakini sisi wote tunahitaji kufanya juhudi zaidi si tu juu ya taka za plastiki lakini kuhusu masuala yote ya bahari. “

Amesema ukweli uko bayana bahari zimechafuka kwani tani milioni 8 za taka za plastiki huishia huko kila mwaka na hatua zisipochukuliwa sasa kubadili hali hiyo basi ifikapo mwaka 2050 taka hizo zitazidi idadi ya samaki baharini.

Cyril Villemain/UNEP
Plastiki zitupwazo kiholela nyingine huishia baharini na kuwa tatizo kubwa kwa viumbe vya baharini.

 

Ameongeza kuwa taka za plastiki hivi sasa zinakutwa hata katika maeneo ya vijijini kabisa katika dunia hii, na zinaua viumbe vya baharini na kuathiri kwa kiasi kikubwa jamii zinazotegemea uvuvi na utalii amesema kwa mfano rundo moja la plastiki kwenye bahari ya Pacif sasa hivi ni kubwa kuliko taifa la Ufaransa. “Sababu tusifanye makossa tuko katika mapmbano , na tunashindwa katika kila kona”
 
 Uvuvi wa kupindukia unamaliza samaki, uchafu unaotoka nchi kavu unasambaratisha fukwe na asilimia 80 ya maji taka yanaelekezwa baharini bila hata kutiwa dawa.Giuterres amesema kana kwamba zahma hiyo haitoshi kuna changamoto nyingine zinazoongezeka za mabadiliko ya tabia nchi ambayo yameongeza kiwango cha kemikali kwenye bahari, joto baharini linafurutu ada na kuua matumbawe na kusababisha vimbunga vya mara kwa mara.

UN siku ya bahari duniani /Renee Capozz
Papa wakiwa wamekusanyika karibu na nchi kavu kwenye kisiwa cha Ufaransa

Ameonya kuwa asilimia 40 ya watu wanaishi karibu sana na pwani na wengi wako hatarini sio tu kutokana na vimbunga bali kupanda kwa kina cha bahari, bali ipia na mmomonyoko wa fukwe. Akisema pamoja na yote hayo “Nashukuru kwamba tuna mkakati wa mpambano, muongozo wetu ni malengo ya maendeleo endelevu SDGs na hususani lengo namba 14 likiwa na vipengee 10 vya kushughulikia kunzia uchafuzi wa bahari na ongezeko la kemikali, kukomesha uvuvi wa kupindukia n ahata kulinda mfumo wa Maisha.”

Siku ya bahari UN/Hoarau Galice
Papa akiwa na mpiga mbizi Bahamas ikionyesha kwamba wakati mwingine viumbe vya bahari vina uhusiano wa karibu na binadamu

Guterres amesema kwenye mkutano wa bahari mwaka, tuliandikisha ahadi zaidi ya 1,300 na ushirikiano.
 “Lakini hakuna hata moja ya mipango hii na maazimio yatakuwa na thamani yoyote kama hatutakubali kwamba tunakabiliwa na dharura ya kimataifa. Na ndiyo sababu nipo hapa leo. Ili kugongakengele, ili kuingiza hisia za hali halisi ya dharura katika maamuzi yenu."
 
Guterres amewakumbusha viongozi hao wa G7 kwamba uongozi wao unahitajika sasa, zaidi kuliko wakati wowote katika kupambana na uchafuzi wa mazingira, katika  kuunda maeneo ya ulinzi wa bahari, katika kufufua uvuvi, katika kujenga mnepo wa mazingira ya pwani na jamii, na hasa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na kuongeza
 “Ikiwa hatutalinda bahari zetu, na kama hatuwezi kushinda vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, mawazo yote ambayo sera zote zinatokana nayo hayatakuwa na maana yoyote.”
 
Kwa hiyo, amewahimiza wote kuchukulia kwa uzito vitisho hivi kwa mazingira ya kimataifa na kuelewa kuwa mustakhbali na usalama wa dunia uko hatarini.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud