Machafuko ya kigaidi yamefurutu ada Sahel:UNOWAS

8 Januari 2020

Mwakilishi wa Umoja wa Mataidfa na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Magharibi na Saleh (UNOWAS) amesema machafuko yanayoambatana na ugaidi yamefurutu anda katika ukanda wa Sahel.

Akitoa ripoti kuhusu hali inayoendelea Sahel kwenye Baraza la Usalama jumatano mwakilishi huyo Mohamed Ibin Chambas mesema “Ukanda huo umeshuhudia mashambulizi mbaya ya kigaidi dhidi ya raia na kulenga vituo na wanajeshi na athari za kibinadamu ni kubwa na za kusikitisha hali ambayo imewavunja nguvu wananchi.”

Idadi ya vifo na majeruhi

Mkuu huyo wa UNOWAS ameyaelezea mashambulizi ya kigaidi  na madhara yake Burkina Fasso, Mali na Niger kuwa yameongezeza kwa moja ya tano  tangu mwaka 2016,kukiorodheshwa vifo zaidi ya 4000 mwaka 2019 pekee  ikilinganishwa na vifo 770 miaka mitatu kabla.

Bwana Chambas ameongeza kuwa “La msingi zaidi mtazamo wa mashambulizi ya kigaidi umebadilika na kuelekea upande wa Mashariki kutoka Mali hadi Burkina Fasso na zaidi na zaidi unatishia mataifa ya Pwani ya afrika Magharibi.

Pia ametakja kwamba idadi ya vifo Burkina Fasso imeongezeka kutoka takriban 80 mwaka 2016 na kufikia zaidi ya 1,800 mwaka jana. Pia hali ya watu kutawanywa imeongezeka mara kumi na kufikia karibu laki 5 mbali ya 25,000 ambao wameomba hifadhi katika nchi nyingine.

Bwana. Chambas ameeeleza kwamba “Mashambulizi ya kigaidi mara nyingi ni juhudi za makusudi za watu wenye itikadi Kali kutaka kushiriki kwenye vitendo haramu ambavyo vinajumuisha kukamata silaha na biashara haramu ya madini.”

Changamoto zinazoingiliana

Ugaidi, uhalifu wa kupangwa na machafuko ya kijamii mara nyingo vinaingiliana hususan katika maeneo ya pembezoni ambako uwepo wa serikali ni dhaifu.  “Katika maeneo hayo watu wenye itikadi kali wanatoa usalama na ulinzi kwa umma pamoja na huduma za kijamii kwa kubadilishana na uungwaji mkono”.amelieleza Baraza Kuu akiunga mkono hoja ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba kwa sababu hizi hatua za kukabiliana na ugaidi  ni lazima zijikite  na kujenga Imani na kuwasaidia watu wa maeneo husika.

Mwakilishi huyo maalu  ameainisha kwamba serikali, wadau, mashirika ya kikanda na Jumuiya ya kimataifa wanakusanya nguvu kutoka kila penmde ya kanda hiyo ili kukabiliana na changamoto hizo.

Tarehe 21 Desemba 2019 mkutano wa wakuu w anchi wa ECOWAS ulipoitisha azimio la mkakati wa 2020-2024 wa kuchukua hatua ili kutokomeza ugaidi katika ukanda huo.

Akiuita huu ni wakati wa kuchukua hatua , Bwana Chambas amesisitiza umuhimu wa kusaidia serikali za kikanda kwa kuweka vipaumbele  kwa mtazamo jumuishi wa viwango mbalimbali na sekta zote.

Akigeukia machafuko baina ya wakulima na wafugaji ambayo ameyataka kuwa ni mabaya zaidi katika eneo hilo Chambas amesema asilimia 70 ya watu wa Afrika Magharibiu wanategemea kilimo na ufugaji kwa kuishi , akisisitiza umuhimu wa kusihi pamoja kwa amani.”Athari za mabadiliko ya tabianchi kwa usalama pia zinasababisha athari mbaya za uhusiano kati ya mabadiliko ya tabianchi na mshikamano wa kijamii, uhamiaji wa kiholela na uhalifu katika baadhi ya maeneo.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter