Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumapili hii, Guinea-Bissau iko tayari kwa uchaguzi wa ‘amani, huru na haki’ – UN

Makao makuu ya Bunge la Guinea-Bissau mjini Bissau.
Alexandre Soares.
Makao makuu ya Bunge la Guinea-Bissau mjini Bissau.

Jumapili hii, Guinea-Bissau iko tayari kwa uchaguzi wa ‘amani, huru na haki’ – UN

Amani na Usalama

Baada ya miezi ya maandalizi, siku moja kabla ya kupiga kura, jumapili hii wapiga kura wote wako tayari kushiriki uchaguzi wa amani, huru na haki, Umoja wa Mataifa umesema leo Jumamosi.

Kwa msaada wa Umoja wa Mataifa, vyama 21 vinachuana kwa ajili ya uongozi wa viti 102 katika Bunge la taifa kwa kipindi cha miaka mine ijayo. Matokeo ya awali yanategemewa kuanza kutangazwa jumatatu.

Kama yalivyo matakwa ya sheria za uchaguzi nchini humo, vyama vyote 21 leo jumamosi vimesitisha shughuli za kampeni. Na ingawa fulana za wagombea zimeendelea kusambazwa na kuvaliwa na wafuasi wao, hakuna sauti za ahadi au hotuba za wagombea zilizosikika.

Akizungumza na UN News mjini Bissau leo jumamosi, Kamishina wa masuala ya siasa, amani na usalama wa kamisheni ya jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, Jenerali Francis Behanzin amesema kuwa “kila kitu kiko tayari”, hali ya usalama “iko sawa” na “kampeni zilifanyika viuri sana.”

Aidha Jenerali Behanzin amesema vyama vinafanya mazungumzo miongoni mwao na hilo akaliita ni jambo zuri kwa demokrasia huko Afrika Magharibi, “Baada ya uchaguzi tutazungumzia changamoto za maendeleo” amehitimisha Henerali Behanzin.

Mwangalizi wa ndani wa uchaguzi wa Guinea-Bissau
Alexandre Soares.
Mwangalizi wa ndani wa uchaguzi wa Guinea-Bissau

 

Waangalizi wa kimataifa kutoka Muungano wa Afrika AU, ECOWAS, Jumuiya ya nchi zinazozungumza kireno CPLP na wengine, wamesambazwa katika maeneo mbalimbali kote nchini.

Msaada wa kitaalamu kutoka Umoja wa Mataifa wakati wote wa mchakato umehusisha mafunzo kwa maafisa wa polisi 80, wanachama wa vyama vya kiraia wapatao 400, maafisa wa uchaguzi 450 na wanahabari 120.

Mwezi uliopita baraza la usalama liliziuru Guinea-Bissau kuangalia na kutathimini hali.