Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni mapenzi yangu kwa mazingira na viumbe yaliyonisukuma kurejeleza bidhaa chakavu-Jonatha Joram

Chupa ambazo awali zilikuwa taka sasa ni mapambo na kila chupa moja  ni dola tano za kimarekani. Hili limewezekana kutokana na ujasiriamali huko Zambia.
UNIC Dar es salaam/Stella Vuzo
Chupa ambazo awali zilikuwa taka sasa ni mapambo na kila chupa moja ni dola tano za kimarekani. Hili limewezekana kutokana na ujasiriamali huko Zambia.

Ni mapenzi yangu kwa mazingira na viumbe yaliyonisukuma kurejeleza bidhaa chakavu-Jonatha Joram

Ukuaji wa Kiuchumi

Ikiwa imesalia takribani miaka kumi kufikia mwaka 2030 ambao umepangwa kuwa ukomo wa utimizaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs ,juhudi kote duniani zinaendelea kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.

Nchini Tanzania, msichana mbunifu Jonatha Joram anayeishi katika jiji la Dar es Salaam ameamua kushiriki katika mchakato huo kupitia utunzaji wa mazingira kwa kurejeleza bidhaa ambazo tayari zimetumika ili ziweze kutumika tena badala ya kutupwa na kuchafua mazingira.

Katika mahojiano haya na UN News, mahojiano ambayo yataendelea kwa kirefu katika makala zetu zijazo,  Jonatha anaeleza jinsi anavyolitekeleza lengo lake la usafi wa mazingira.

Endelea kufuatilia matangazo yetu ya siku zijazo ambapo utasikia kwa kirefu juhudi za Jonatha Joram katika utunzaji wa mazingira nchini Tanzania.