WFP na serikali ya Myanmar wafanya ushirikiano mpya kutokomeza njaa

Makazi ya wakazi wa kata ya Aung Mingalar mji wa Sittwe, jimbo la Rakhine, Myanmar.
OCHA/P.Peron
Makazi ya wakazi wa kata ya Aung Mingalar mji wa Sittwe, jimbo la Rakhine, Myanmar.

WFP na serikali ya Myanmar wafanya ushirikiano mpya kutokomeza njaa

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP na serikali ya Myanmar wametia saini makubaliano mapya kwa lengo la kutokomeza njaa. U Than Aung Kyaw,  mkurugenzi mkuu katika idara ya mambo ya nje  na Stephen Anderson mkurugenzi wa WFP nchini Myanmar ndio waliosaini makubaliano kati ya pande hizo mbili.