Mafunzo ya roboti nchini Uganda yanafungua upeo wa watoto wa Shule 

23 Disemba 2019

Kutana na Solomon Kingi Benge mwanzilishi wa kituo cha mafunzo ya trknolojia ya roboti  .Ameamua kuusambaza ujuzi wake kwa wanafunzi katika shule nchini Uganda.

Huyo ni Solomoni akisema fursa za Maisha ziko chungu tele kikwazo pekee ni ukomo wa fikra zako, ana umri wa miaka 35 kutoka mjini Kampala.

 

Alianzisha kituo kiitwachop Fundiboti kituo ambacho hutumia mafunzo ya roboti katika kuunda na kuhamasisha kizazi kipya kuwa watatuzi wa matatizo na wabunifu kwa msaada wa Benki ya dunia. Lakini safari yake ilianza vipi?“Nilipokuwa mtoto nilipenda sana masuala ya umeme, nilipenda sana masuala ya teknolojia na nilitaka kuelewa vyema jinsi gani dunia inavyofanya kazi. Na kwa bahati mbaya shule ikawa ni sehemu tu ya kukariri kwa ajili ya mitihani na kusoma kwa ajili ya kufaulu.”

Solomon anasema hali hiyo ilimchanganya na alipofikia umri wa barubaru akaanza kufikiria kuanzisha mahali ambapo vijana waliokuwa na fikra za teknolojia kama zake wanakuja kufundishwa, kupewa muongozo na kujifunza kufikia upeo wa yale wanayoweza kubuni na kuyafanya , "Kwa kushuhudia tekinolojia na kujifunza, hii inamaanisha watoto hawa wanawezeshwa kubuni na kuamini katika mustakbali ambao watautaka. Lakini cha msingi zaidi kinawapa ujuzi ambao wanauhitaji kuweza kuishi katika kizazi kijacho. Tunapaswa kujifunza kuwa wabunifu kwa rasilimali tulizonazo."

Kwa msaada wa Benki ya Dunia Solomon anataka kufundisha vijana wengi zaidi Afrika na anaamini kwamba bara la Afrika linaweza kuwa na mafanikio makubwa kupitia vipaji vya vijana wake.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter