Pengo la usawa ndio mtihani wetu katika vita dhidi ya UKIMWI:UNAIDS

26 Novemba 2019

Jumla watu milioni 24.6 walikuwa wanapata matibabu dhidi ya virusi vya UKIMWI, VVU,  hadi Juni mwaka 2019 kwa mujibu wa ripoti mpya ya  ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya UKIMWI, UNAIDS iliyiozindulwa hii leo nchini Kenya. Hata hiyo ripoti hiyo inasema kuwa watu milioni 32 wamepoteza maisha kote dunia tangu ugonjwa huo ugunduliwe. 

Ripoti hiyo iliyoziduliwa leo mjini Thika nchini Kenya inasema kwa mwaka 2018 takribani watu milioni 37 walikuwa waanishia na virudi vya ukimwi. Milioni 36 wakiwa na watu wazima huku wengine takriban milioni 1.7 wakiwa ni watot walio chini ya miaka 15. Akizindua ripoti hiyo mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Winnie Byanyima alisema kuwa kile kinahitaji kufanywa kwanza ni kuhakikisha kuwa kila mmoja alieyeambukizwa na virusi vya UKIMWI amepata huduma bora, 

(Sauti ya Winnie Byanyuma)

Ripoti hiyo pia inasema hadi mwisho wa mwezi Juni mwaka 2019 watu milioni 24.5 walikuwa wanapata madawa ya ARV kutoka watu milioni 7.7 mwaka 2010. Lakini hata hivyo bado watu wengi wanoishi na VVU wanakumbwa na unyanyapaa jinsi anavyosema Josephene Wanjiku ambaye aligundua kuwa na virusi hivyo mwaka 1990.

(Sauti ya Josephine Wanjiku)

Kwa mujibu wa ripoti ni kuwa mwaka 2018 asilimia 62 ya watu wote wanaoishi na VVU walikuwa wanapata matibabu. Hata hivyo ilisema kuwa hadi sasa watu milioni 74.9 wameambukizwa tangu kuzuka kwa janga hilo. Huku milioni 32 wakiwa wamefariki dunia hadi sasa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud