Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikundi vya kijamii vyatumika kusambaza dawa za kupunguza makali ya VVU katika maeneo ya vijijini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI yanaendelea kote duniani
UNDP video
Mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI yanaendelea kote duniani

Vikundi vya kijamii vyatumika kusambaza dawa za kupunguza makali ya VVU katika maeneo ya vijijini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Afya

Katika mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI, VVU na UKIMWI nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, vikundi vya kijamii vinavyoundwa na watu wanaoishi na VVU vinasaidia kusambaza dawa katika maeneo ambayo yana ugumu wa kufikiwa kutokana na usalama mdogo na uhaba wa huduma za kiafya, juhudi ambazo zimewasaidia wengi kama ilivyo katika vijiji vya Zemio. 

Ni video zilizopigwa kwa ndege isiyo na rubani zinaonesha eneo la mji mdogo wa Zemio katika Jamhuri ya Afrika ya kati. Katika maeneo ya ndani kusinimashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, ni misafara michache inayoweza kupita na hivyo upatikanaji misaada ni mgumu. Miundombinu haipo na vituo vya ukaguzi visivyo rasmi vinasimamiwa na watu wenye silaha.

Kwasababu ya mgogoro wa mwaka 2017 kati ya makundi yenye silaha, zaidi ya watu elfu 40 wamefurushwa katika makazi yao. Takribani watu elfu 30 wanaishi katika nchi za jirani za Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Marina amekuwa akiishi na Virusi Vya UKIMWI tangu mwaka 2010. Miaka miwili iliyopita aliondoka nchini mwake kwasababu ya mapigano. Pamoja na ukosefu wa usalama, amerejea Zemio miezi miwili iliyopita ili aweze kupata matibabu.

Siyo wengi ambao wamekuwa na bahati. Kutonana na kutengwa na pia kutawanywa kwa watu, eneo la Haut Mbomou ambako ndiko Zemio ilipo, kuna viwango vya juu vya maambukizi ya VVU kwa nchini CAR, asilimia 12 mara tatu zaidi ya maeneo mengine ya nchi.

“Kabla, nilikuwa imara na afya kwasababu ya matibabu. Kwasababu ya vurugu, nilikimbilia DRC. Hatukuwa na chakula, ilikuwa vigumu. Sikuweza kumeza dawa. Hapo ndipo lipoanza kuumwa tena. Kiasi cha maambuki kikawa juu.”

Farcre ni mwakilishi wa kikundi kinachojiita ‘Community ARV Group’ kilichoanzishwa na Madaktari wasio na mipaka  kinachounndwa na watu wanaoishi na VVU ambao wanaishi kwa kusaidiana.

Fiarcre kwa ajili ya wenzake, anaendesha baiskeli kuja katika Hospitali ya Zemio kuchukua dawa za miezi sita za kufubaza Virusi Vya UKIMWI. Anaiokoa gharama za wengine kwa safari za kuja hospital. Baada ya kuupokea mzigo, anapimwa damu kabla ya kuondoka“Manesi wamekuja kuja kunipima kiasi cha virusi katika damu.  Kwa sasa havionekani.”

Katika mwaka uliopita, kati ya wanachama wa kundi hilo 700, asilimia 80 yao wote walipimwa na kuonekna kuwa virusi vimedhibitiwa kiasi cha kutoonekana, kutokana na matibabu wanayoyapata.

Mtu anayeishi na VVU anayemeza kwa usahihi dawa za kufubaza VVU yaani ARVs kama Fiacre anakuwa na kiasi kidogo cha maambuki kiasi cha kufanya virusi visionekane.

Juhudi za jamii, nyingi ambazo zinafanywa na watu wanaoishi na VVU, zimesaidia sana katika mapambano dhidi ya VVU duniani kote. Kwa UNAIDS, kuimarisha na kuwasaidia ni muhimu ili kuhakikisha mapambano dhidi ya VVU yanaendelea kuwa ya msingi.

Shirika la Umoja wa Mtaifa linalohusika na UKIMWI, UNAIDS inakadiria kuwa kwa mwaka jana wa 2018, watu milioni 37.9 duniani kote walikuwa wanaishi na VV, milioni 24 walikuwa wanapokea matibabu, watu milioni 1.7 walipata maambukizi mpya huku watu 770,000 walifariki dunia kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI.

Watu milioni 32 wamefariki dunia kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI tangu kugundulika kwa ugonjwa huu.