Skip to main content

Chuja:

#VVU

Utepe mwekundu- ishara ya kimataifa ya kampeni ya kupambana na VVU na UKIMWI
Public Health Alliance/Ukraine

Elimu ya afya ya uzazi haipaswi kuwa aibu – Tumaini Community Services Mbeya Tanzania 

Nchini Tanzania, Shirika la Tumaini Community Services linatekeleza mradi wa ‘Dreams’ yaani ‘Ndoto’ katika wilaya ya Mbeya mjini, Kyela na Mbarari mkoani Mbeya kwa ufadhili wa mfuko wa rais wa Marekani wa harakati za kupambamba na UKIMWI, PEPFAR kanda ya Tanzania, lengo likiwa kuwawezesha vijana balehe elimu ya afya ya uzazi, elimu ya kujitambua na elimu ya kiuchumi ili kupunguza maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI.

Sauti
2'50"
Public Health Alliance/Ukraine

Sindano mpya ya Cabotegravir ni habari njema katika vita dhidi ya VVU

Shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa za tiba kwa gharama nafuu, UNITAID limetangaza utekelezaji wa mchakato mkubwa wa uvumbuzi wa hivi karibuni katika kuzuia virusi vya ukimwi ,VVU ambao ni sindano mpya ambayo inachukua wiki nane kabla ya muathirika kupewa dozi nyingine badala ya tembe anazopaswa kumeza kila siku.

Sauti
2'25"

22 Machi 2022

Yaliyomo Jaridani la Jumanne Machi 22, 2022- Ujenzi wa mabwawa waboresha maisha ya wakulima wa mbogamboga nchini Rwanda.

-Sindano mpya ya Cabotegravir kutusaidia kukinga wengi dhidi ya VVU:UNITAID.

-UNHCR inahitaji dola bilioni 1.2 kwa ajili ya ktoa msaada kwa wakimbizi milioni 2.3.

Makala imeangazia mjadala wa wakulima wadogo wadogo kutoka Afrika.

Sauti
14'28"
Mwanaume akipima VVU kwenye kituo kimoja cha afya huko Odienné, nchini Côte d’Ivoire.
© UNICEF/Frank Dejongh

Sindano mpya ya Cabotegravir kusaidia kukinga wengi dhidi ya  VVU:UNITAID 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa za tiba kwa gharama nafuu, UNITAID limetangaza utekelezaji wa mchakato mkubwa wa uvumbuzi wa hivi karibuni katika kuzuia virusi vya ukimwi ,VVU ambao ni sindano mpya  ambayo inachukua wiki nane kabla ya muathirika kupewa dozi nyingine badala ya tembe anazopaswa kumeza kila siku.

Sauti
2'25"
Utepe mwekundu- ishara ya kimataifa ya kampeni ya kupambana na VVU na UKIMWI
Public Health Alliance/Ukraine

Ninaishi na VVU lakini nina afya njema na uwezo mkubwa wa kazi. Msitubague - Wu Megnam

Shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO limeendelea mara zote kuhamasisha mazingira mazuri ya kazi ikiwemo kutokuwepo kwa ubaguzi au unyanyapaa kwa wafanyakazi kutokana na hali zao iwe ulemavu au ugonjwa.  Kisa hiki cha  Wu Mengnan wa China, ambaye miaka 15 iliyopita yeye na mumewe walipimwa na kukutwa na Virusi Vya UKIMWI, VVU kinaonesha kuwa bado kuna haja ya kufanya zaidi ili kukomesha ubaguzi na unyanyapaa mahali pa kazi au wakati wa kutafuta ajira. Taarifa ya Anold Kayanda inaeleza zaidi.

UNICEF/Frank Dejongh

UNITAID waomba ufadhili zaidi wa vifaa vya kujipima VVU

Kuelekea kilele cha siku ya UKIMWI Duniani hapo kesho Desemba 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa za tiba kwa gharama nafuu, UNITAID limesema usumbufu na ucheleweshaji wa huduma za VVU unaosababishwa na janga la COVID-19 ulisababisha kupungua kwa vifaa vya upimaji na utambuzi wa VVU kwa kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kuonekana ndani ya miongo miwili.

Sauti
2'28"