Ajira milioni 8 zahitajika ukanda wa Afrika Mashariki kila mwaka- UNECA

8 Novemba 2019

Ajira milioni 8 zinahitajika kila mwaka katika ukanda wa Afrika Mashariki, ukanda ambao unaelezwa kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi ni kubwa mno kuliko kanda nyingine barani Afrika.

Mkutano wa mwaka wa tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika, UNECA ukiwa umekunja jamvi huko Asmara, mji mkuu wa Eritrea, imeelezwa kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki ni kubwa mno na haiendani na kiwango cha uzalishaji wa ajira, wakati huu ambapo takwimu zinaonesha kuwa ajira milioni 8 zinahitajika kwenye ukanda huo kila  mwaka.

Kulikoni basi na nini kifanyike? Priscilla Lecomte wa Umoja wa Mataifa ambaye ameshiriki mkutano huo amezungumza na Vincent Leyaro, Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam nchini Tanzania ambaye anaanza kwa kuelezea sababu.

 

 

UN/Partners Tags: 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud