Skip to main content

Rushwa isipodhibitiwa soko huru Afrika litasuasua

Picha:UNCTAD
Mwanamke mchuuzi wa samaki.

Rushwa isipodhibitiwa soko huru Afrika litasuasua

Ukuaji wa Kiuchumi

Macho na masikio yanaelekezwa Rwanda hapo kesho ambako kunatarajiwa kutiwa saini makubaliano ya kuwa na eneo la biashara huria barani Afrika.

Vikwazo visivyo vya forodha ni miongoni mwa mambo yanayopaswa kuangaziwa barani Afrika ili soko huru tarajiwa barani humo, CFTA, liweze kufanikiwa, amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga. John Kibego na maelezo zaidi.

Akihojiwa na Priscilla Lecomte wa Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Afrika, ECA huko Kigali Rwanda, kando mwa mkutano wa kamati tendaji ya Muungano wa Afrika, AU, Balozi Mahiga ametaja vikwazo hivyo kuwa ni..

(Sauti ya Balozi Augustine Mahiga)

Naye Stephen Karingi, mkuu wa idara ya muungano wa kikanda ya ECA, amesema kuundwa kwa eneo huru la biashara barani Afrika kutatoa fursa nyingi kwa wafanyabiashara lakini pia…

 (Sauti ya Stephen Karingi)

“ CFTA itatoa fursa kubwa pia za ajira, hasa kwa vijana wa Afrika. Kwa sababu biashara ya kikanda, inayofanyika kati ya nchi za Afrika, kwa zaidi ya asilimia 40 ni bidhaa za viwanda. Bidhaa hizi zinahitaji nguvu kazi zaidi. Kwa upande mwingine, nchi zikifanya biashara na nchi zingine duniani, nchi za Afrika zinauza zaidi mafuta ama madini, ambazo ni bidhaa zisizohitaji nguvu kazi sana. Kwa hiyo, wanachama wa Umoja wa Afrika watakaposaini CFTA, watasababisha ongezeko la biashara ya kikanda, ambayo itachangia katika kuimarisha sekta ya viwanda na kutoa fursa za ajira kwa watu wengi zaidi.”

Nchi zote 55 za bara la Afrika zinatarajia kukubaliana juu ya kuunda CFTA wiki hii ambapo mkataba huo unatarajiwa kutiwa saini kesho na utaanza kutumika iwapo nchi zaidi ya 22 zitauidhinisha.