Ubunifu wetu utasaidia kunusuru bahari- Nancy Iraba
Tukiwa bado kwenye mkutano huo wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari, mbali ya kikao cha ngazi ya juu cha viongozi makundi mbalimbali yalianza kukutana mwishoni mwa wiki likiwemo kongamano la vijana. Nancy Iraba mwanasayansi wa masuala ya bahari kutoka chou kikuu cha Dar es salaam nchini Tanzania ni miongoni mwa wanaohudhuria kongamano hilo la vijana na bahari akiwakilisha taifa lake.