WFP yapeleka msaada kwa familia zilizoathirika na mafuriko nchini Somalia

1 Novemba 2019

Mvua kubwa isiyo ya kawaida na mafuriko yamezidi kukumba Somalia, Sudan Kusini na Kenya mwaka huu. Watabiri wa hali ya hewa wanatarajia mvua hiyo kubwa kuendelea kunyesha hadi Desemba.

Nchini Somalia, katika wilaya ya Beletweyne na sehemu zingine zimeathirika vibaya na mahitaji ya kibinadamu ni makubwa.

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linashirikiana kwa karibu na wizara ya inayohusika na masuala ya kibinadamu na majanga nchini Somalia na pia mashirika mengine ya serikali.

Tayari WFP imetuma helikopta kusaidia shughuli za kibinadamu kati ya Beletweyne na sehemu zilizo karibu zilizoathiriwa vibaya na mafuriko kutoka mto Shabelle.

WFP ina mpango wa kusaidia familia 4,000 kutoka vijiji saba kwenye wilaya ya Beletweyne. Pia itapeleka tani 24 ya biskuti  kwa njia ya helkopta ikifanya safari kadhaa kwenda Beletweyne.

Karibu tani 20 za biskuti zimesafirishwa kutoka Mogadishu kwenda Baidoa kwa njia ya barabara na pia kwenda mji wa Bardale ulio kusini magharibi kwa njia ya ndege.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud